WAKAAZI WA MTWARA WA MSAKA HALIMA MDEE WATAKA AFUTE KAULI

KUFUATIA taarifa iliyotolewa na Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee kuhusu utoaji wa ardhi kwa bilionea Alhaji Aliko Dangote, wakazi wa kijiji cha Mgao, Halmashauri ya Mtwara Vijijini wamemtaka kufuta kauli yake.


Wakitoa malalamiko yao kwa vyombo vya habari, baadhi ya wakazi wa kijiji hicho ambao walijitambulisha kwa majina ya Seif Said na Mohamed Njiti, walisema kuwa kitendo cha ardhi yao kulinganishwa na kaniki na kipande cha kanga kimewasikitisha.


Walisema uthamini wa ardhi umeshaanza, wanatarajia kulipwa Sh milioni 10 kwa ekari moja, huku wakipata malipo ya mimea iliyopo kwenye mashamba yao, zoezi ambalo bado linaendelea katika maeneo ya vijiji vya Kisiwa na Mgao.


Kwa upade wake, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Abdulahman Shaha, alisema amesikitishwa na taarifa iliyotolewa kwa kulinganisha ardhi yao na kipande cha kaniki.


“Ile kauli sio sahihi, ilibidi aje Mgao apate taarifa sahihi ili akatoe bungeni, sisi tuko katika tathmini ya ardhi, kila mwananchi atalipwa stahiki yake, walipaji wa ardhi hii ni Mamlaka ya Bandari Tanzania siyo Dangote,” alisema Shaha.


Naye Meneja wa Mamlaka ya Bandari Mkoa wa Mtwara, Hebel Mwasenga, alisema mamlaka hiyo inamiliki eneo la hekta 1,000, ambapo mwekezaji huyo amepewa eneo la hekta 25 kwa ajili ya ujenzi wa bandari ndogo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company