Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akilakiwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofika kwenye viwanja vya Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Chamwino Ikulu, wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma Juni 22.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akiangalia kikundi cha ngoma za asili wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Chamwino Ikulu, wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma Juni 22.2015, kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho. (DK)
Mzee Aidan Mazego (kushoto), akitoa salamu za baraka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati) alipofika kwenye Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Chamwino Ikulu, wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma Juni 22.2015, kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kulia ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Dodoma, Mzee William Kusila.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Chamwino Ikulu, Joseph Seganje kuhusu Mnara wa kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyeishi katika kijiji hicho, kuanzia Julai 10.1971 hadi Oktoba 30.1971 akihimiza siasa ya ujamaa na kujitegemea nchi nzima, wakati Waziri Membe alipofika wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma Juni 22.2015, kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wa pili (kushoto) ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Janeth Mashele.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akisoma falsafa za Mwl. Nyerere alipotembelea Mnara wa kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyeishi katika Kijiji cha Chamwino Ikulu, kuanzia Julai 10.1971 hadi Oktoba 30.1971 akihimiza siasa ya ujamaa na kujitegemea nchi nzima, wakati Waziri Membe alipofika wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma Juni 22.2015, kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wa tatu (kushoto) ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Janeth Mashele.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akitazama picha za matukio mbalimbali ya Mwl. Nyerere alipotembelea Mnara wa kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyeishi katika Kijiji cha Chamwino Ikulu, kuanzia Julai 10.1971 hadi Oktoba 30.1971 akihimiza siasa ya ujamaa na kujitegemea nchi nzima, wakati Waziri Membe alipofika wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma Juni 22.2015, kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kushoto ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Dodoma, Mzee William Kusila na (wa tatu kushoto) ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Janeth Mashele.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago