Mwendesha mashtaka wa Misri, Hisham Barakat auawa kwenye shambulio la bomu jijini Cairo

Baadhi ya viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood ambao hivi karibuni mwendesha mashtaka Hisham Barakat aliiomba mahakama iwahukumu adhabu ya kifo
Reuters
Na Emmanuel Richard Makundi

Mwendesha mashtaka wa Serikali ya Misri, Hisham Barakat amefariki dunia akiwa hospitalini, saa chache tu baada ya msafara wake kushambuliwa kwa bomu jijini Cairo, leo Jumatatu.

Akiongea na waandishi wa habari, jijini Cairo, waziri wa sheria, Ahmed al-Zind amethibitisha akiwa hospitalini, kuwa mwendesha mashtaka, Barakat amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.

Tangazo hili linatolewa saa chache tu baada ya kuripotiwa kushambuliwa kwa msafara wa mwendesha mashataka huyo ambapo watu kadhaa waliuawa huku yeye pamoja na maofisa wake wengine wakijeruhiwa kwenye shambulio hili.

Bomu hilo liliharibu majengo kadhaa pamoja na magaro yaliyokuwa jirani kwenye eneo la Heliopolis ambapo kwa mujibu wa polisi magari zaidi ya matano yaliharibiwa vibaya.

Msafara wa Hisham Barakat ulishambuliwa wakati yeye pamoja na walinzi wake walipokuwa wakielekea kwenye makao makuu ya ofisi yake jijini Cairo.

Shambulio hili limetekelezwa saa chache baada ya tangazo la wapiganaji wa kiislamu nchini humo kutangaza vita dhidi ya wafanyakazi wa mahakama hasa majaji ambao wamekuwa wakitoa hukumu kali dhidi ya wafuasi wa kiislamu wa Muslim Brotherhood.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company