Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji jijini Dar es salaa pamoja na mkoa wa Pwani kwa kutumia mashine za BVR lililokuwa linategemewa kuanza rasmi tarehe 4.7.2015 jijini Dar es salaam na 25.06.205 kwa mkoa wa Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo Habari, NEC imesema imeahirisha zoezi hilo kutokana na kuchelewa vifa vya uboreshaji kutoka mikoani ambako zoezi hilo linaendelea pamoja na vifaa vilivyokuwa vinakusudiwa kuanza kutumia Dar es salaam kupelekwa katika mikoa ambayo wananchi wamejitokeza kwa idadi kubwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Hata hivyo tume hiyo imewataka wananchi kuwa watulivu wakati vifaa vikisubiriwa kutoka mikoani.
Kwa habari zaidi soma hapa taarifa kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago