Misikiti minane kufungwa Tunisia

Misikiti minane kufungwa Tunisia

Utawala nchini Tunisia unasema kuwa utafunga misikiti minane wiki moja inayokuja kwa madai kwa inachochea ghasia.

Hii ni kufuatia shambulizi lililofanyika kwenye hoteli moja ambapo watu 39 wengi wao wakiwa raia wa kigeni waliuawa na mwanamme mmoja aliyedanganya kuwa mtalii.

Kundi la islamic state lilisema kuwa ndilo lililotekeleza shambulizi hilo.

Waziri mkuu nchini Tunisia Hanib Essid anasema kuwa baadhi ya misikiti ilikuwa ikitumika kueneza propaganda na kuunga mkono ugaidi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company