Mpiganaji wa Dola la Kiislam akishikilia bendera nyeusi ya Islamic State, karibu nampaka wa Iraq na Syria.
ALBARAKA NEWS / AFP
Na RFI
Zaidi ya nchi ishirini za muungano dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu unaoongozwa na Marekani, zinakutana Jumanne wiki hii katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.
Mkutano huu unafanyika baada ya siku kadhaa wapiganaji wa Islamic State kuidhibiti miji ya Palmyra nchini Syria na Ramadi nchini Iraq.
" Hakutakuwa na maswali yatakayoutia matatani muungano dhidi ya Islamic State ", chanzo cha kidiplomasia cha Ufaransa kimehakikisha. Hata kama wapiganaji wa Islamic State wameendelea kupata ushindi siku za hivi karibuni nchini Iraq na Syria, mkakati utasalia ule ule. Mashambulizi ya anga na kutoa msaada kwa vikosi vya ardhini vya jeshi la Iraq na wapiganaji wa Kikurdi vitaendelea.
Wakati huu ni muhimu kwa Ufaransa na washirika wake kuuchunguza mkakati wao, kwa mujibu wa mtafiti David Rigoulet-Roze wa Taasisi ya Ufaransa ya Uchambuzi wa mikakati (IFAS).
" Kunatakiwa mkakati huo uchunguzwe na kutazama namna ya kuupitia upya ili nchi nchi za muungano zisiendelei kubaki kwenye kampeni ya mashambulizi ya angani pekee. Kuna idadi ya vigezo vya ziada ambavyo vinapaswa kuzingatia, mapoja na kutoa matatani masuala mengine, hasa juu ya suala la wajibu wa Iran, ambayo ni muhimu kwa vile Iran inashiriki moja kwa moja katika vita vya ardhini dhidi ya Islamic State, hasa nchini Iraq. Kwa hiyo, kunaona kuwa kuna utata wa kile kinachoitwa muungano. Nchi wanachama wa muungano dhidi ya Islamic State zinaichukulia Iran kuwa ni adui. Na hii pengine ni moja ya maelezo ya kushindwa kutekelezwa kwa mkakati hadi sasa. Muungano huu unauundwa na nchi ambazo hazina maslahi sawa au kwamba zina maslahi tofauti. Na hali hii ndiyo inayokwamisha mafanikio ya mkakati huu dhidi Daech ", amesema David Rigoulet-roze .
Nchi za muungano pia zitazungumzia idadi kubwa ya wanajihadi wa kigeni ambao wanaendelea kuwa kwenye safu ya Islamic State. Nchi hizi zitajadili ufadhili wa kundi hili lenye msimamo mkali wa kidini. Pia kwenye ajenda kutazungumziwa "mawasiliano ya kimkakati", kufuatia maneno yanayotumiwa na kundi hili kwa kuwavutia watu kujiunga nalo.
Hatimaye, nchi za muungano pia zitatathmini suala tete linalopelekea jamii mbili za Wasuni na Washia kutoelewana, na kujaribu kutia pande hizo pamoja, hususan kuboresha maridhiano kati ya pande hizi mbili.
Mkutano huo utaongozwa na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, waziri mkuu wa Iraq Haïdar al-Abadi na waziri wa mamabo ya nje wa Marekani John Kerry. Lakini John Kerry hatokuwepo katika mkutano huo kutokana na majeraha aliyoyapata kutokana na ajali ya baskeli.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago