Waziri wa mambo ya nje ya Marekani John Kerry |
Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani waziri Kerry ametoa pongezi hizo kwa niaba ya Rais Barack Obama na watu wa Marekani.
Taarifa imesema wakati Rais John Pombe Magufuli na uongozi wake wanaanza kuwajibika, Marekani inatarajia kuendeleza na kusimarisha ushirikiano wake baina ya nchi hizo mbili wakati wanafanyakazi pamoja kusaidia katika tamaduni za kidemokrasia , kuchochea usalama wa kieneo, na kuhamasisha maendeleo ya kicuhumi.
Rais Mteule John Magufuli akiapishwa
Pia amesmshukuru rais anayeondoka madarakani Jakaya Mrisho Kikwete katika juhudi zake kusaidia kujenga uhusiano bora baina ya Marekani na Tanzania.
Hata hivyo Marekani inaendelea kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu tangazo la maafisa wa tume ya uchaguzi kuonyesha nia ya kubatilisha uchaguzi wa Zanzibar.
Imetoa wito kwa utawala mpya wa Tanzania kuhakikisha kuwa matarajio ya watu wa Zanzibar yanafikiwa kwa wakati, haki na amani katika kukamilisha mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar.