Watoto 48 waokolewa, Ivory Coast

Mtoto akifanya kazi katika shamba la Kakao

Watoto wapatao 48 wameokolewa katika mashamba ya Kakao walikokuwa wakitumikishwa kusini Magharibi mwa Ivory Coast.

Shirika la Kimataifa la Polisi la Interpol limesema pia limewakamata wafanyabiashara wa magendo 22.

Watoto hao wenye miaka kuanzia mitano mpaka 16, wametoka Burkina Faso, Guinea, Mali na pia kaskazini mwa Ivory Coast.

Shirika hilo limesema baadhi ya watoto walikuwa wakifanya kazi katika mashamba hayo kama watumwa wakiwa na hali mbaya, bila ya malipo wala kusoma shule.

Polisi mia mbili nchini Ivory Coast walishiriki katika operesheni hiyo ya uokozi, iliyoratibiwa na Interpol pamoja na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM).

Operesheni hiyo ni ya kwanza ya aina yake katika nchi za Afrika magharibi na maeneo mengine.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company