Hii ndiyo Historia ya John Magufuli wa CCM

Chama tawala nchini Tanzania Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza daktari John Magufuli kuwa mgombea wake

Chama tawala nchini Tanzania Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza daktari John Magufuli kuwa mgombea wake wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa ujao.

Daktari John Magufuli, alisajili asilimia 87 % ya kura za wajumbe, hiyo ikiwa ni kura 2104.

Daktari John Magufuli, aliwashinda wapinzani wake Bi Amina Salulm Ali na dakta Asha-Rose Migir.

Magufuli ni Nani?

Lakini je Daktari John Magufuli ni Nani? Daktari John Magufuli ni Nani?

Mgombea wa urais wa chama cha CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania.

Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera.

Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.

Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.

Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT .

Alizaliwa Oktoba 1959Alianza siasa mwaka 1995

Alipohitimu, daktari Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge.

Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu.

Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.

Alianza siasa mwaka 1995

Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.

Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi.Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti

Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.

Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.

Anatambulika kuwa Mchapa kazi

Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti.

Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.

Na alipokuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Bwana John Magufuli alikwenda hadi bandari ya Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina iliyokuwa inashukiwa kufanya uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya Tanzania.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company