Serikali ya zamani ya Nigeria kuchunguzwa juu ya ufisadi

Taarifa hizo zinakuja baada ya baraza hilo kupinga kutekelezwa kwa ahadi zilizotolewa na rais Buhari wakati wa kampeni ,kutoa dola 25 kwa mwezi kwa vijana ambao hawana ajira kwa lengo la kupunguza kiwango kikubwa cha kutokuwa na ajira.
Rais wa zamani wa Nigeria, Goodluck Jonathan akiwa pamoja na rais aliye madarakani sasa, Muhammadu Buhari mjini Abuja, Nigeria
Baraza la senate la Nigeria limeutaka utawala wa rais Muhammadu Buhari kuanza haraka uchunguzi wa serikali ya rais wa zamani Goodluck Jonathan, ili kurejesha fedha ziloibiwa kutoka kwenye miradi ya kutokomeza umasikini, ikiwemo mradi unaojulikana kama Subsidy Reinvestment and Empowement Program au SURE-P kwa kifupi.

Baraza hilo la senate linaeleza kuwa serikali ya zamani lazima iwajibishwe kwa fedha zilotumia kutekeleza miradi ya SURE-P na miradi mingine ya kutokomeza umasikini.

Taarifa hizo zinakuja baada ya baraza hilo kupinga kutekelezwa kwa ahadi zilizotolewa na rais Buhari wakati wa kampeni ,kutoa dola 25 kwa mwezi kwa vijana ambao hawana ajira kwa lengo la kupunguza kiwango kikubwa cha kutokuwa na ajira.

Christopher Kolade mwenyekiti wa zamani wa SURE-P alijiuzulu wadhifa wake mwaka 2013, akisema mradi huo umekosa uwaminifu wake kutokana ulaji rushwa na uingiliaji kati wa kisiasa.

Seneta shehu Sani mwenyekiti wa kamati ya senate katika kamati madeni ya nje na ndani , anasema kuna ishara kuwa baadhi ya maafisa katika utawala ulopita walitumia miradi ya kutokomeza umasikini, kwa ajili ya kujitajirisha wenyewe.

Bw. Sani anasema, hii inatokana na ripoti kuhusu ulaji rushwa na udanganyifu ambao ulitokea wakati wa utawala wa rais wa zamani Goodluck Jonathan. Tumehisi njia bora Zaidi ya kutenda haki ni kufanya uchunguzi huu, wa ulaji rushwa na udanganyifu uliofanyika, hususan program inayojulikana kama SURE-P, ili serikali ya sasa iweze kurudisha fedha zilizoibiwa.

Lakini maseneta kutoka chama cha upinzani cha Peoples Democratic Party PDP walipinga uchunguzi huo. Wanasema rais Buhari anaonekana kuwa hajajiandaa vyema kutatuwa changamoto za kijamii na kiuchumi na atatumia uchunguzi huo kuleta mvuto wa uwezo wake wa kuongoza. Wamesema serikali inastahili kusonga mbela badala ya kutafuta kushitaki maafisa waliopita. Sani anasema utawala uliopo madarakani umewaahidi wanigeria kupambana na ulaji rushwa wote na kurudisha serikalini fedha ziloibiwa. Wito wa baraza la senate kufanya uchunguzi huo, anasema Bw Sani, ni sambamba na ahadi ya utawala wa Buhari.
CHANZO VOA SWAHILI
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company