Sudan Kusini: zaidi ya watu 36 wapoteza maisha katika ajali ya ndege ya mizigo

Picha ya eneo ambapo watu wasiopungua 27 walipoteza maisha Novemba 3, 2015 mjini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, katika ajali ya ndege ya mizigo iliyoanguka ikipaa angani katika eneo la kilimo.
AFP/AFP           Na RFI

Zaidi ya watu 36 wamepoteza maisha Jumatano hii mjini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, ambapo ndege ya mizigo imenguka kwenye ikipaa angani katika eneo la kilimo.

Ndege imenguka katika kisiwa kidogo cha White Nile, kilomita mbili kutoka uwanja wa ndege. "Hadi sasa miili 36 imechukuliwa" na Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Sudan Kusini, Majju Hillary, mkuu wa mawasiliano wa shirika hilo, ameliambia shirika la habri la Ufaransa la AFP.

" Hatuwezi kuhakikisha kwamba hii ndio idadi kamili, kwa sababu baadhi ya vipande vya ndege ni vizito kwa kuvinyanyua na kuviweka upande wa pili wa kisiwa. Kwa hiyo kunahitajika vifaa vya kutosha ili kukabiliana na hali inayojiri eneo hilo ", Majju Hillary ameongeza.

Watu wawili wamenusurika lakini mmoja wao amefariki baada ya kuokolewa, Hillary amesema.

Sababu halisi ya ajali hazijulikani kwa sasa. Katika kisiwa hicho, ambapo waandishi wa habari wa AFP, wametembelea sehemu ya mkia mweupe wa ndege umekua katika eneo la msitu. Vipande vingine vimeteketea. Mabaki, ikiwa ni pamoja na bawa na kipande cha chumba cha marubani na wasaidizi wao kimekua kwenye sehemu ya ardhi huku miili ya watu ikitapaka katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa chanzo cvha kidiplomasia cha Armrnia, "Waarmenia watano, ambao ni wafanyakazi wa ndege hiyo ilioangika nchni Sudan Kusini, ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha."

Kwa mujibu wa redio za Sudani Kusini, ndege ilianguka wakati ambapo ilikua ikipa angani ikiwa njiani kuelekea Paloich, kilomita 600 Kaskazini mwa Sudan Kusini, katika jimbo la Upper Nile, moja ya maeneo ya mapigano makubwa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe yanayoiathiri nchi hiyo tangu Desemba 2013.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company