AJTC NA DISKO TOTO,MZIKI WA ZIMWA, FUJO ZATAWALA.


Side alimanusura kupoteza jicho,tuubiri tamko la chuo.

Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha hiyo jana walidhiirisha wazi ya kwamba  kunguru afugiki walA shwala awezi jenga ushirika na samba.
Hayo yote yalijiri baada ya wnachuo hao kushindwa kudhiirisha ya kwamba jitiada za muda mrefu zilizolenga kuwazuia na kuwanyima kupata disko ni batili.

Kwa mara ya kwanza walipewa kibali cha kuburudika kwa muziki kuazia jioni hadi majogoo yaani asubuhi lakini walishindwa kuutumia mwanya huo kwa usitaarabu.

Kwani disko hilo lililazimika kusitishwa majira ya saa 8 usiku baada ya wanafunzi kushindwa kutii wito wa kuacha vitendo vya kipuuzi ikiwemo fujo,katika kurupushani hizo zilizo wawia ugumu baadhi ya viongozi kuzituliza akiwemo kiongozi wa Michezo mwenye cheo cha uwaziri Chalesi King Didasi naibu wake,waziri wafedha Kevo alimaarufu kama baba Price na Raisi wa chuo hicho David PaTriki.

Baya zaidi mwanafunzi wa darasa la mkomanzi aitwae Saidi maarufu kama side alijeruhiwa vibaya na alimanusura kupoteza uwezo wajicho lake kuona,mwanafunzi huyo alichomwa vibaya na kitu chenye ncha kali chini ya jicho lake.

Aliemfanyia unyama huo hakuweza kutambulika lake ila kwa mujibu wa mashuhuda watukio hilo wanadai ya kwamba alikuwa amesuka nywele na sio mwanafunzi.

Sherehe hiyo ilifanyika kwa shabaha ya kuwakarisha wanafunzi wageni wakiwemo walianza mapema mwaka huu na mwishoni mwakajana kwa ngazi zote za cheti na stashahada, na sherehe hiyo yaaina yake ilifanyaka kwenye ukumbi mpya uliopo mita zaidi ya miatano kutoka eneo la viwanja vya chuo.

Bado mwandishi wa blogu hii anaendelea kufwatilia kwa karibu zaidi ili kukujuza kwaundani …na jitiada za kumtafuta mwalimu mlezi wa wanafunzi hao Bw. Andrea Ngoboleau naibu wake Neema Mwaipele ili kutuelezea zaidi na tamko lake zinaendelea.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company