Na Oscar Samba.
Hakika tabia yoyote ile iliombaya haiwapendezi wengi na
aifanyae punde anapotendewa basi huwa mkali na kukasirika kwa hili sinabudi
kuuruhusu huu msemo usemao mtendwa
akitendwa huisi kaonewa kuchukuwa nafasi yake.
Kwa wale wote wenye tabia za wizi wa aina yoyote yaani uwe
waunyanganyi,uviziaji ama ule wakuaminiwa kuacha tabia kama hizo mara moja
kwani kwakufanya hivyo watakuwa wamejiepusha na madhara kama
vile kupigwa au kupoteza maisha.
Mfano mwaka jana jijini Daresalam katika kata ya kigogo
nilishuhudia kijana mmoja aitwae Kristofa akipokea kipigo kikali kutoka kwa
watu wenye hasira kali na hatimae kupoteza maisha yake.
Katika kata hiyo hiyo kijana mwingine alikatwa masikio yake na
kwa bahati nyingine alipata mwanya wa kukurupuka mbio na hatimae kutokomea
kusiko julika lakini alibakia kama nyoka kwani
ndie kiumbe anaeishi kwa mwonekano wakutokuwa na masikio.
Mbali na hayo yote pia unaweza kupoteza ndugu jamaa na
marafiki sanjari na kujikuta ukiishi maisha kama
kisiwa ni kimaanisha kutengwa.
Ningumu mtu kama huyu kuaminiwa
na mtu yoyote hususani wale wanaotambua vikali tabia zake na waswahili hunena
tabia ningozi wakimaanisha haifichiki kwa hiyo hata kwa wale wasio zifahamu
kiunaga ubaga tabia zake nirahisi kuzichukulia hatua punde pale zitakapo
ziirika.
Kwa nini uhishi kwa tabu zote hizo? embu chukua uamuzi wa
busara fanya sasa maamuzi sahihi achana na wizi,na kuhaidi na ninakuhakikishia
kuwa maisha bila wizi yanawezekana.
Tabia nyingine ni hii
ya lugha chafu nikimaanisha matusi,wapo watu tena wengi ambao vinywa vyao
vimetawaliwa na maneno ambayo hata shetani akiyasikia anashanga hawajali wapo
wapi ni nani anaewazunguka, mkubwa wala mdogo?
Ukisafiri na magari ya umma hususani haya ya masafa mafupi
wahudumu wake [makonda] sanjari na
madereva wake wametwaliwa na matusi ya hali ya juu sio hawo tu bali hata wale
wapigadebe hususani wanao patikana kwenye vituo vikubwa kwa vidogo.
Kunawale wanajiita wamepinda na maisha kwao bangi,mirungi ni
kama maji na ndivyo matusi yanavyo zidi
kuendelea kuwa sehemu ya falisafa na itikadi ovu maishani mwao.
Wengine bila kujua au kujitambua wameanza kuiga huku wakiona
yakwamba ni fasheni ama ndiko kwenda na wakati,kijana eti ili aonekane ni
mjanja basi anajilazimu kuongea sentesi mbili kisha anachanganya na upuuzi
huwo.
Wapo ambao kwa kuzoe basi atakapo jikwaa ama kusahau kitu
kiunganishi kama sio kikumbushio ni bonge la
tusi.
Sio matusi tu bali hata lugha za kebei na dharau zimekuwa ni
kero kwa wengi,binadamu wenzetu hawana lugha za hekima kwao neno samahani ni
msalaba mzito usio kuwa na mbebaji wala mtushwaji,hawa ndo wale ambao kama
mkiwa kwenye msongamano au daladala na kwa bahati mbaya ukamkanyaga basi
kinachotoka kinyani mwake ni bonge la msonyo,kwa lugha ya kebei na jicho la
uchokozi utaangaliwa.
Kwa bahati nyingine utangulize samahani basi kitakachokukmba
ni majibu ya karaha kama vile “hiyo samahani
yako inanisaidia nini?,”hakika huo sio ustaarabu.
Kama nilivyo tangulia ya kwamba wao kuomba radhi ni wagumu sana kama sio wao tu basi
hata miongoni mwetu tungali tupo.Unapo mkosea mwenzaka na amini ni kwa bahati
mbaya haunabudi kuhakikisha ya kwamba unatanguliza msamaha kwani neon nisamehe
hupunguza jaziba na huleta upendo huku likizidi kumuaminisha mtendwa ya kwamba
katendwa kwa bahati mbaya tu nasio kusudio.
Ndugu zanguni mkiwemo wale wafanya biashra wadogo wadogo na
wakubwa ambo baadhi yao
wanapoulizwa bei hujibu kwa hasira ,au wanapo ombwa kupunguza bei za bidhaa zao
mfano “nimesema ni shilingi mia tatu” au …. “usikii au weweni kiziwi..unataka
nunua utaki ondoka..uza na wewe?
Bila kumungunya maneno na waambia ya kwamba tabia kama hizo
hazifai hamnabudi kuziacha mara mmoja tumieni lugha nzuri na nyororo bila
kujali unaeongea nae ni rafiki au adui ni mtukanaji au muungwana kwani huenda
akaacha tabia zake ovu kwa kuvutiwa na maneno laini na murwa kutoka kinywani mwako.
Majungu hii ni sifa mbaya ambayo inazidi kukumbatiwa na watu wengi hususani maofisini na popote pale
penye mikusanyiko ama mafanikio.
Kuna watu wengi hakika
wananishangaza kama sio kunisitajabisha kazi yao kubwa ni umbea na ajira
yao kuu ni majungu,kila uchwao hawa wazi kuwatendea wenzao mema bali hukaa kitako,wima;
wakitafakari na kutunga mipango batili ya kuwaribia wenzao.
Vipaji vyao vikubwa ni uongo na ushekunaku,wafanyakazi wapo
radhi kutengeneza majungum dhidi ya mfanyakaziu wenzao ili tu aonekane ni mbaya
kwa bossi na usoni mwa wengine.
Unapo fanikiwa wafanyakazi au wasanii pia jamii inayo
kuzunguka ni rahisi kuketi na kuanda mipango ambayo huishia katika kuunda
skendo za uzushi dhumuni lao kubwa likiwa kukukatisha tama.
Tabia hizi siinzuri katika haya hatuna budi kujirekebisha
kwani tusipo fanya hivyo mwisho wa ubaya sikuzote ni aibu hakika ewe ambe
uliazimia kuendelea na unajisi huwo iposiki utaaibika vikali,hususani pale
ukweli utakapo amua kujitenda na uongo.
Pia huvunja moyo wautendaji kazi kwani mtu huweza
kukwazika,watu hukuchukia kituambacho kitakupelekea kuwa na marafiki wachache
na punde upatapo shida ni vigumu kupata msaada.
Utatengwa na wenzako ukizingatia hawatapenda kukuhusisha au kukushirikisha
kwenye mazungumzo yao
yaaina yoyote.
Mavazi, sio dada zetu peke ambao wanaendeleaa kuwa kumzo kwe
kila kona za miji bali siku hizi hata kaka zetu nao wanazidi kutia, fora
utawakuta wamevalia mavazi yao
nusu makalio huku wakitembea kwa mienendo ya kunesa nesa bega moja liko juu
jingine lina niginia na hatua za madaa.
Nguo wanazo vaa licha ya kuwa nyembamba kamachupa pia hutoa
mwanya kwa kila apishananae kuona mazazi mengine yaliopo ndani, kwa kuwa ni
nusu makalio basi utaona bukuta zimejipanga kama
ngazi na hatimae ya mwisho ni ile nguo ndogo.
Unamuonesha nani upuuzi huwo? sina mengi kwako bali ni
kwambialo ni hili; jirekebishe, achana
na ushamba huo.
Ni ruhusu ni wareje dada zetu,hawa bila kuwaonea ni kwamba
wamekuwa ni kituko tena cha ajabu,kama ni pepo basi limeaga na kama ni jinni hakika limefanikiwa na
inawezekana ni shetani basi yangu imani ni kwamba anawafwasi wengi.
Haieleweki labula wewe mweenzangu unaweza kunisaidia katika
hili,kwa kifupi hawa dada zetu mavazi wanayo ya vaa hayana tija sio kwao tu
bali hata kwa jamii kwa ujumla na kama wao wananufaika na mitoko hiyo basi
amanufaa yao ni yale yasio kuwa na maendeleo.
Hakuna ubishi katika hili ya kwamba hayupo mwanaume yoyote
ambae huweza kumpenda kwa dhati mwanamke ambae hajiheshimu katika mavazi yake
na ndio maana wengi wao huishia kuchezewa tu.
Usisitajabu upitapoa barabarani na kumkuta binti wa watu
amevalia nguo ya nusu mwili inayo acha kitovu nje,mapaja juu juu an mengine
hayana hata ushuhuda yana fanana nay a kunguru miguu mwemba,pia kwa wale wanao
vaa suruali basi utawaonea hata huruma na kubakia ukijiuliza.
Ninaamini kabisa nguo nyingne huvaliwa kwa kujikaza na zipo
ambazo hawawezi kuzi vaa bila msaada wa shosti wake alikadhalika zile ambazo
huvaliwa kwa kupakwa sabuni na kuzitoa ndio mbinde kwani ni nyembamba mno.
Jirekebishe ewe mwanadada anza kujisitiri sasa achana na
nguo za fedheha acha kuwa gumzo mitaani kwa kuwapa watu mitaji ya kukujadili,na
inaweza ikawa nisababu ya wewe kuto kuolewa au mpendwa wako kutotaka kuongozana
na wewe pia ndio maana mahusiano yenu yana legalega au kuto kudumu.
Hata kama ni mke wa mtu heshi basi ndoa yako kwa
kujisitiri,mpe furaha mumeo ya kudiriki kutoka na wewe pia ajivunie kukutambulisha
na kujinafasi kwa marafiki zake.
Unajua ni kwa nini kwa mkwe hawa kupendi? Achakujiuliza sana jibu lake ni rahisi sana,mwonekano.
Ni yangu matumaini ya kwamba utakuwa chachu ya kuchukia kwa
kuacha na kuwaonya wale wote watendao mabaya, kwa leo sina mengi na kusihi
uendele kufwatilia ukurasa huu wa jirekebishe pamoja na kurasa nyingine,tafadhali
nipe kibali cha kuhitimisha..asante.