Na Oscar Samba
Siku chache zilizopita Raisi wa Tanzania Mh. Jakaya pamoja na viongozi wengine wandamzi na baadhi ya wanasiasa akiwemo Mh.Jemsi Mbatia ambae ni mwenyekiti wa NCCR Taifa na mbunge waliwataka watanzania kuendelea na moyo wa uzalendo unaoamini kuwa kila rasilimali inayopatikana ni mali ya taifa zima.
Sina lengo la kupingana na hoja hiyo moja kwa moja wala kuunga mkono kama ilivyo bila kueleza kiunagaubaka,pia kundi la pili linaloongozwa na wanasiasa wakiwemo wengi kutoka vyama pinzani ikiwemo CHADEMA na baadhi ya watu hususani walio wazawa waeneo husika zilipo patikana rasilimali ameonesha misimamo na mitazamotofauti na hiyo.
Ikumbukwe kwamba siku chache zilizopitaza mwishoni mwa mwaka jana baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mtwara waliandamana kwa dhumuni la kushindikiza wape kipaumbe cha kunufaika na gesi iliogunduliwa mkoani huko.Malala miko hayo yalikuja mara baada ya serikali kutangaza kwamba itajenga bomba la gesi litakalo toka mkoani hapo hadi Dar es salaam kwa ajili ya kusafirisha maligafi hiyo ili ikafuliwe na kuzalisha umme katika jiji hilo.
Wanachi hao walipinga dhana hiyo na kuiona nidhalimu kwa madai ya kwamba wanahitaji kiwanda cha kufua gesi hiyo kijengwe mkoani kwao iliwawe wakwanza kunufaika na rasilimali yao wanayo ita baraka kutika kwa Mungu.
Wengine walienda mbali kidogo na kudokeza kuwa wakati Raisi anazindua gesi hiyo aliwahaidi kuwa kiwanda au mitambo hiyo ingalijengwa Mtwara.Wazawa hawa wanaamini ya kwamba kama kutajengwa viwanda vingi ni dhairi shairi kwamba ajira itaongezeka na pia watapata huduma ya umeme kiuraisi tofautu na hivi sasa.
Kwa upande wake serikali na TANESCO wanadai kwamba gesi hiyo inaitajika sana mkoani Dar es salamu ili kusaidia viwanda vingi ambavyo vipo mkoani hapo na itasaidia kuokoa mabilioni ya shilingi yanayo tumiwa na shirika hilo katika kuzalisha umeme wa dharura unaotumia mafuta mazito.
Wakijibu hoja hii baadhi ya wananchi wakishirikiana na wanaharakati tofauti na wasomi wanadai kwamba gesi hiyo inaweza kufuliwa Mkoani Mtwara na hatimae umeme kuingizwa kwenye gridi ya Taifa na hatimae kutumika paka Dar es salam,wengine wakadokeza kwamba kuna gesi iliogunduliwa pwani kwani nini? gesi hii isingali safirishwa hadi mkoani hapo ukizingatia kwamba Pwani na Dar ni karibu kuliko Mtwara au Lindi ambako pia kuna gesi.
Wapo walioendelea kudokeza akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kasikaziuni Zitto Kabwe ya kwamba kuna gesi ambayo huenda ikagundulika Wilayani Temeke jiji Dar es salamu ambayo huenda ikawa ni nyingi kulikoile ya mkoani Mtwara ambayo ni futi za ujazo trilioni 16,kama mambo ni hivyo wanaendelea kuhoji ni kwanini serikali isingeendelea kuvuta subira au ikaamua kutumia rasilimali nyinginezo ziizipo karibu?
Yote kwa yote wao pinga dhana hii wanatumia kisingizio cha kwamba rasili mali yoyote inayogunduliwa mahalipopote Tanzania ni mali ya Taifa zima toka henzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa rasimali ya mkoa au wilaya haitumikikimaeneo,hata Raisi Kikwete katika kusisitiza hilo kwenye hutuba yake ya mwisho wa mwenzi wa mwisho wa mwaka jana alisema”rasilimali yoyote inayogunduliwa hapa nchini ni mali ya taifa zima na sio eneo ilipo gunduliwa,..mfano mkoa wa Dar es salaam unatoa asilimia 80 ya mapato yote ya taifa’’ laki Mh. Rais alisahau kwamba miundombinu mizuri ya serikali na uma yaani barabara ,mashule na hata hosipitali ikiwemo ya taifa vyote vipo Dar es salaam.
Pia wanao kubali au wanao tetea hoja hiyo wanadai pia matumizi ya umme katika mikoa ya Lindi na Mtwara ni megawatti 84 lakini wanashindwa kufikiri na kukumbuka kuwa ni asilimia ya 20 tu ya wakazi wa alimashauriya wa Mtwara Mjini ndio wenye huduma hiyo kwa maana kwamba kama wakazi wote au asilimia kubwa wakipata huduma hiyo na itaji litaongezeka.
Na ikumbukwe sio watu wa Mtwara peke yao la hasha! Bali malalamiko kama hayo yapo sehemu nyingi nchini ikiwemo wakulima kulia kwani wao ndio wazalishaji wakuu wa chakula na kilimo ndio uti wa mkongo wa uchumi wa taifa letu huku kikitoa ajira kwa watanzania wengi ,wanalalamiakia miundombinu mibovu na kuto kudhaminiwa kama wale wa mijini.
Sasa hoja yao kubwa ni hii ya kwamba ifike wakati nao wanufaike zaidi na rasilimali zinazotoka katika maeneoyao kimaendeleo kuliko kuendelea kuambulia madhara tuu kama wale waoishio katika maeneo yaliogunduliwa madini ya Urenium ambao wameshaaza kuachwa na ulemavu wakudumu na magomjwa ya ngozi huku macho yao yakidhoofu.
Ikumbukwe sia lengo langu kujenga uadui,kupuuza ma wazo ya watu,kuchochea na kuamsha ghadhabu zilizo lala wala kudhofisha na kuua moyo wa uzalende miongoni mwa watanzania,narudia tena sio lengolangu wala shabaha yangu,ila kusema ukweli sio dhambi bali dhambi ni kuficha maovu na kukaa kimia kwa mwamvuli wakuto kuvunja amani na kuendelea kukumbatia baadhi ya viini macho vilivyo na faida kwa wache na wajanja tuu,huku walio duni wakiendelea kuwa duni zaidi hususani wale wa vjijini wanaoendelea kufanywa utali,wakiwemo wamang’ati.
NI NI NA NILIPI LENGO NA DHUMUNI LANGU,
Jibu la swali hilo dogo lakini makini linakuja kama lifwatavyo;wito wangu kwa serikali ni kwamba hiakikishe kila sehemu inapopatikana rasilimali inawanufaisha wazawa nasio kukimbila sehemu nyingine huku eneo husika likibaki utupu na kuendeleza ule usemi sugu wa Zitto usemao rasilimali laana,inawezekana labla unashanga mantiki ya msemo huwo, ngoja nikupe mifano ifwatayo…
Wakazi wa eneo la ifadhi ya Taifa Ngorongoro hivi sasa wanasumbuliwa na baa la njaa na kwa mujibu wa hosipitali ya Katoliki ya Enduleni watoto 14 mwaka jana walilazwa hosipitalini hapo kutokana na utapia mlo.
Mei mwaka juzi watoto zaidi ya 1,000 waliugua ugonjwa wasurua na kati yao 200 walifariki, ukweli unaeleza kwamba idadi hiyo isinge tokea kama watoto hao wangalikuwa na afya bora ambayo imepuputishwa na njaa kali pia kuto kupewa chanjo ya ugonjwa huwo ikiwa ni sababu nyemelezi.
Sasa embu tujiulize katika eneola uridhi wa dunia watu wanapoteza maisha eti! Kwa sababu ya njaa angali eneo hilo huzalisha au uliingizia taifa zaidi ya sh. Bilioni 54 kwa kupata fedha za kigeni dola milioni 50 katika kipindi cha juni mwaka jana.Cha ajabu serikali imeshindwa kusambaza chakula (mahindi) tani 3,600 kutoka kwenye gala la taifa ilikukabiliana na tatizohilo,huku dhamani yake ikiwa ni sh.milioni 315 tu !embu nisaidie kufanya hesabu ya kiasi cha fedha nilicho kupa hapo juu ingawa ni cha kipindi kichache kwa kutoa na dhamani ya fedha zilizo itajika ili kusambaza chakula hicho.
Je,kwa watu kama hawa na kwa mazingira kama hayo ya faa nini kujivunia uwepo wa rasilimali iliopo katika maeneo yao ang’ali bado tena wanazidi kusumbuliwa kwa kuto kuitajika katika eneo hili?,hiyo sio hoja mpya ingawaje kwa leo sii hitaji kujadili sentensi hiyo tafadhali naomba tuendelee….
Kwa maeneeo kama ya Mererani,Muadui kule mkoano Shinyanga,Mara wilayani Tarime kwenye mgodi wa Goldeni Mara na kungineko wakazi wake walicho na wanachonendelea kuambulia ni mashimo ya migodi,magonjwa ya sioeleweka yanayo sababishwa na kemiko mbali mbali uharibifu mkubwa wa mazingira na kubaki kunyanyasika kwa kuishi bila miundombinu ya maji,umeme na hata elimu.
Hauamini tembelea maeneo hayo leo ukianza na Mererani hakika utapigwa na putwa kwani watoto wanaenda shule katika mazingira magumu ya kimavazi,hata majengo yenyewe ya kiwa ni choka mbaya au hohehahe.
Matukio ya ubakaji wizi uliokidhiri na hata kama hujui matumizi ya madawa ya kulevia au haujawai kuona mirungi na bangi basi tembelea maeneo hayo hakika utavijua vyote hivyo.
Watu wanaishi kama vile hakuna sheria,hivi ni kweli serikali imeshindwa kuboresha maeneo hayo?na moyo wa uzalendo pindi unapotokomea kunakojulikana ni nani wakujitwisha la wama?
Jibu lake ni gumu katika swali hilo ni rahisi lisilohitaji hata punje moja ya ncha ya upeo wa kufikiri na kutafakari.
Hainiingi akilini kwa TRA kukimbilia kukusanya kodi tena wakiwa kwenye mashangingi na magari mengineyo ya kifahari bila serikali kuwajali wazawa wamaeneo hayo ambayo mgonjwa akiugua hupelekwa hosipitali kwa vikapu au machela za kamba na magogo,mikokoteni ndizo ‘’ambulance’’zao na magari ya punda.
Cha ajabu watu wa maeneo mengine ikiwemo Masaki, Mbezi Beach na Magogoni bila kusahau Mjengoni marufu hivi sasa kama “paradiso ndogo’’ wakiendelea kuneemeka huku vyanzo vya mapesa hayo vikiendelea kuwa duni.
Naupande wa piiwa shlingiwanaendelea kuzifisadi na kuzikimbiza Uswizi na kuwaacha masikini tunao waita wa Mungu wakiendelea kutaabika kwa kujisukumia kwenye mikokoteni na matrekita ya kulima punde watakapo kwenda mijini.
Nasisitiza tena na tena ya faa sana kila eneo nchini likapata keki sawa ya taifa na kuepuka upendeleo na sio dhambi maeneo yanayo toa rasilimali nyingi kupewa kipaumbele japo kiduchu ya rasilimali zinazo patikana na tuepukane na ahadi uchwara zisizo tekelezwa ikiwemo ile ya kujenga kiwanda cha mbole ya chumvi chumvi mkoani Mtwara ingawaje yule bilionea wa Afrika ambae ni maarufu huko Afrika ya Magharibi kama Bwana saruji alisha hadi kufanya hivyo, lakini imani ya wanamtwara inazidi kuyayuka na sio Mtwara tu bali katika kona mbali mbali za nchi yetu ingawaje mimi ninauita ugonjwa sugu wa bara letu lakini na chechemea kuungana na swali na hoja ya Zitto isemayo “rasilimali laana” .
Nimesheheni mengi lakini tutaendelera kuhabarishana na ningependa kuitimisha kwa kuiomba jamii kutokuwa mstari wa nyuma kutetea haki zao hususani mambo yale yenye kubeba na kulenga mustakali mzima wa maisha yao ya leo na kesho.
Serikali hiache kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu na badala yake ifanye tafiti za kutosha katika kujibu hoja na kabla ya kuruhusu mianya ya hoja hizi, pia waache uhuni wakuamua maswala yao juu kwa juu wakiwa ,Ikulu ama barabarani tena Dar bila kuwashirisha wananchi yaani wazawa.
Mfano mkubwa ikiwa ni swala hili la kujenga hilo bommba la gesi limeamuliwa na kupitishwa na kupigiwa upatu na serikali kuu bila hata kuwashirikisha wanachi wa eneo hilo pia mabalozi wa nyumba zao wakibaki wakitokwa na miayo kwa kutokujua nini na ni kwa nini hawaku hojiwa hata kwa kebei.
Mwisho kabisa ninaomba hekima ya hali ya juu itumike katika kuda haki kama hizi ili kuto kujenga matabaka na mipasuko baina yetu na tuendele kutamani rasilimali zetu zitunufaishe sote lakini kwa usawa na haki na kumbuka hakuna haki bila wajibu.
Na nina chelae kuungana na G.Lema aliewahi kusema ya kuwa haki haiombwi bali hudaiwa.
Wanasiasa hususani wa upinzani ni ruksa kulifanya swala hili kuwa mitaji ya kisisa na kuendelea kusaka umaarufu kwani hakuna asietaka hayo bali angalizo kubwa liwe ni misingi ya haki,usawa,uzalendo na mchunge umoja wakitaifa.Tafadhali endelea kutembelea blog hii kwa makala zaidi, na tarifa moto motoi asante kwa ushirikiano wbko.