MISIRI KWA CHAFUKA

Kumetokea ghasia katika mji wenye bandari wa Misri, Port Said, baada ya mahakama kutoa hukumu ya kifo kwa washtakiwa 21 kuhusu ghasia zilizotokea kwenye mechi mwaka jana.
maandamano ya Port Said
Watu kama 16 wameuwawa pamoja na askari polisi wawili na wengine kama 50 wameumia.
Ghasia hizo zilianza baada ya wafuasi wa washtakiwa kupambana na polisi nje ya gereza wanamozuwiliwa.
Jeshi sasa limetumwa hapo.
Mwaka jana ghasia kwenye kandanda ziliuwa watu kama 70 baada ya mechi baina ya klabu ya Port Said na ile kutoka Cairo.
Polisi walilaumiwa kuwa hawakufanya kitu kuzuwia fujo hizo za mwaka jana.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company