Isabel dos Santos, bintiye Rais
wa Angola Jose Eduardo Dos Santos, amekuwa mwanamke wa kwa kwanza wa
Afrika kuwa Bilionea . Hii ni kwa mujibu wa jarida la kiuchumi nchini
Marekani la Forbes.
Bi Isabel mwenye umri wa miaka 40 anamiliki hisa
katika makampuni kadhaa nchini Portugal, ikiwemo kampuni moja ya
televisheni na benki moja nchini Angola.Hisa hizo zote zimefikisha mali anayomiliki kuwa na thamani ya mabilioni na hivyo kumuweka kwenye orodha ya watu wengine wanaomiliki mabilioni barani Afrika.
Isabel Dos Santos
- Alifungua mkahawa wa Miami Beach akiwa na umri wa miaka 24
- Anamiliki asilimia 28.8 za hisa ya kampuni ya habari ya Zon, ambayo ina thamani ya dola milioni 385
- Anamiliki aslimia 19.5 ya hisa za benki ya Banco BPI, yenye thamani ya dola milioni 465
- Asilimia 25 ya hisa za benki ya Angola, Banco BIC, yenye thamni ya dola milioni 160
- Anadaiwa kumiliki asilimia 25 ya kampuni ya mawasiliano ya Angola ya Unitel...
Watu wengi nchini Angola , nchi yenye utajiri mkubwa, wanaishi kwa kipato cha chini ya dola mbili kwa siku.
Angola inajitahidi kukabiliana na athari za vita vya wenywe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 27, baada ya nchi hiyo kujipatia uhuru wake kutoka kwa Portugal.
Alisomea uhandisi katika chuo kikuu cha King's College mjini London, ambako alilelewa na mamake.
Vita vya Angola vilikamilika mwaka 2002 na nchi hiyo imeweza kuibuka kama mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika,pamoja na kuwa uchumi wake unakuwa kwa kasi .
Familia ya Rais Jose Eduardo Dos Santos ambaye amekua mamlakani kwa miaka 33 , inadhibiti sehemu kubwa ya uchumi wa nchi hiyo.
Duru zinasema kuwa Bi dos Santosa hapendi sana kujionyesha hadharani licha ya kufanikiwa sana kibiashara.
Tangu mwaka kuanza biashara yake ya mkahawa, mjini, Luanda, mwaka 1997, amekuwa mfanyabiashara mwenye ushawishi mkubwa nchini Angola na Portugal.
Akiwa na asilimia 28.8 ya hisa katika kampuni ya Zon, yeye ni mwanachama wa bodi ya kampuni hiyo na mmiliki mkubwa wa hisa zake , kulingana na Forbes.