TCRA yaonya watumiaji wa simu za mkononi


MAMLAKA ya Udhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imetoa hadhari kwa watumiaji wa mitandao ya simu za mkononi kuwa makini na wizi unaofanywa kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu.
Udanganyifu unaofanywa kwa wenye simu kutumiwa ujumbe unahitaji kutuma fedha kwa ajili ya kulipia gharama za huduma kwa njia ya mtandao huku anayetumiwa fedha hizo bila kufahamika.
Mkurugenzi wa Watumiaji na watoa huduma za Mawasiliano, Dk. Raymond Mfungahema alitoa taarifa hiyo wakati akitoa mada ya kazi za TCRA kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia.
Alisema wateja wengi wamekuwa wakitumiwa ujumbe, unaowataka watume fedha kwa watu wasiowajuwa wakiamini kuwa wanatuma fedha hizo kwa kampuni za simu, jambo ambalo si kweli. Alisisitiza kwamba kampuni zote za simu, zina namba zao za utambulisho kwa ajili ya mawasiliano ya aina yoyote.
“Utakuta mmiliki wa simu anatumiwa ujumbe ili atume kiasi cha fedha kwa mtu asiyemjua, huku asitambue anatuma fedha hizo kwa ajili ya kulipia huduma gani. Wateja wanatakiwa kubaini aina hii ya wizi kwa njia ya mitandao ya simu,” alisema.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Sauda Mtondoo aliiomba TCRA kutilia mkazo uelimishaji umma, kunapotokea changamoto za matumizi ya huduma mbalimbali zilizo chini ya mamlaka ili kuwaongezea uelewa watumiaji.
Alitaka mamlaka ibane kampuni za mawasiliano ya simu, zinazobuni utaratibu wa kujipatia fedha kwa njia za kutaka watumiaji wa simu za mkononi kuingia katika utumaji wa fedha kwa njia ya ujumbe mfupi ilihali huduma hiyo siyo lazima kwa wateja.
Aliitaja mfano wa huduma hizo za kuchangia fedha ni pamoja na nyimbo
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company