Alianzia hapa.www.hakileo. blogspot.com |
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ni mtu wa vituko vingi na amekuwa akitoa burudani iwe ni kwa maneno yake kuhusu baadhi ya mada za soka au vitendo vyake anapokuwa uwanjani.
Mara nyingi Kocha huyu huwa na kitabu kidogo na kalamu ambavyo huwa anavitumia kuandika vitu alivyoviona toka kwa wachezaji wake abavyo anatarajia kuvizungumza wakati wa mapumziko ili kujaribu kuleta mabadiliko .
Kwenye mchezo dhidi ya Man United Mourinho aliona kitu ambacho alitaka kuandika lakini tatizo alikuwa amesahau mahali alikoiweka peni yake na ilimchukua karibu dakika nzima kuitafuta peni hiyo mpaka alipoipata.