- UBAKAJI ULIOHALALISHWA HUFANYIKA MBELE YA MASHUHUDA
Bi. Arodia Gebasaki ambaye ni mjane akisimulia jinsi mila ya kutakasa wajane inavyofanyika kwa mwandishi wa makala haya (hayupo pichani) ambapo yeye alikataa kufanyiwa mila hiyo na hakuna madhara yoyote aliyopata tangu kufiwa na mume wake, miaka 14 iliyopita
Baadhi ya wajane wakiwa katika picha ya pamoja na mwandishi wa makala haya baada ya kufanya mahojiano kuhusu mila ya kutakasa wajane wilayani Ukerewe, Mwanza. Wajane hao wameipiga vita mila hiyo kutokana na kumdhalilisha mwanamke.
MWANDISHI Reuben Kagaruki
"Udhalilishaji huu uliojificha katika mila inayoitwa Okusomboka kwa
Wakerewe ni tendo ambalo hufanyika kwa maana ya kuhitimisha uhusiano wa ndoa
kati ya mume na mke aliyefiwa. Mila hiyo huhitaji uhusiano huo uhitimiswe hivyo
sababu ulianzishwa kwa tendo la ndoa.BIBI a l i b a kwa , mama akabakwa, dada
amebakwa na mke wangu atabakwa nitakapofariki.”
Huo ndiyo uhalifu mkubwa uliojificha
kwenye mila ya Okusomboka (kutakasa) kwa wakazi wa Ukerewe hasa kwa Wakara na
Wajita.Kwa Wakerewe ubakaji ni jambo la
kawaida na unatukuzwa kwa mikono miwili kupitia mila ya Okusombaka.
Hayo ndiyo maisha ya kawaida kwa wakazi
wa Ukerewe mkoani Mwanza wanaotukuza ubakaji, mbakaji anapomaliza tendo hilo, wakati mwingine
anashangiliwa kwa kupigiwa vigelegele na akina mama akionekana shujaa wa
kuondoa watu mikosi kupitia ubakaji, ingawa wao hutafsiri kuwa wanasomboka.
Ubakaji huo kupitia mila ya Okusomboka
ni sehemu ya maisha ya kawaida kwa wakazi wa Ukerewe na unaheshimiwa kiasi
kwamba wale wanaokataa kubakwa wanatengwa na kunyooshewa vidole kila
wanapopita.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili
wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza juu ya mila ya Okusomboka (utakasaji)
umebainisha vitendo vya ubakaji vimekuwa vikitendeka tangu enzi na enzi na
kuingia katika karne hii ya sayansi na teknolojia.
Ambapo ubakaji huo, unalenga wanawake wajane na unafanyika
siku ya nne ya matanga tangu kutokea kifo cha mwanaume ndani ya familia.Bila kujali uchungu anaokuwa nao mjane wa kupoteza mume
wake, anatafutiwa mbakaji (Omwesya-yaani mtakasaji) ambaye anakodiwa na kulipwa
ujira ili kutekeleza kitendo hicho cha kubaka mjane, ambacho kwa Ukerewe ni cha
heshima, katika kuhitimisha uhusiano kati ya mume aliyekufa na mjane aliyebaki.
Ingawa sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya Mwaka 1998 inatoa
adhabu kali kwa watu wanaopatikana na hatia ya makosa ya ubakaji, kwa Ukerewe
hawajui kama Okusomboka ni kubaka, hivyo
kukiuka wazi wazi sheria hiyo inayotolewa kwa watu wanaofanya vitendo hivyo.
Ubakaji unafanyika kwa uwazi na wameenda mbele zaidi kwani
kuna watu maalumu ambao wanalipwa fedha na wakati mwingine hata mifugo kwa
ajili ya kuwabaka wanawake wanaofiwa na waume zao kwa hoja kwamba wanatimiza
sharti la mila hiyo.
Mbakaji kabla ya kuanza kitendo hicho, huwa anaandaliwa
chakula maalumu ikiwemo pombe ambayo huwa anakunywa na kuchangamka na hapo
ndipo anaaza kubaka.
Kutokana na hali hiyo wanawake wengi walioolewa wilayani
Ukerewe ni wabakwaji watarajiwa na wale watakao kataa kubakwa, basi wajiandae
kutengwa na ndugu, kunyooshewa vidole na jamii inayowazunguka na mali za
marehemu waume zao kutotolewa urithi.
Pia, mjane anayekataa kutakaswa ajiandae kutopata mwanaume
wa kumuoa.
Vi kwa z o h i v y o , n d i v y o vinavyowashinikiza
wakubali kubakwa na watu maalumu ambao hukodiwa kwa fedha au kulipwa mifungo
kwa ajili ya kubaka wajane.
Katika mila hii, mwanamke analazimishwa kufanya tendo la
ndoa bila ridhaa yake tena na mtu asiyemfahamu na haandaliwi kwa namna yoyote
ile kwa ajili ya tendo hilo.
Wakati kwenye majumba ya utakasaji unafanyikwa kwa njia ya
maombi, kwa Ukerewe unafanyika kwa njia ya ubakaji.
Okusomboka ni tendo la ndoa linalohusisha watu wawili, mjane
ambaye amefiwa na mume au mke na mwingine ambaye yupo kwa ajili ya kazi hiyo.
Mfano leo hii ikitokea mwanamke akafiwa na mume wake, baada
ya mazishi yanafanyika matanga ambapo siku ya nne ya matanga, anakodiwa mtu
kutoka miongoni mwa watu wanaokodishwa kwa ajili ya kutakasa mjane na kufanya naye
tendo la ndoa tena bila hiari ya mjane.
Ubakaji uliojificha kwenye mila ya Okusomboka (kutakasa) kwa
Wakerewe ni tendo ambalo linafanyika kwa maana ya kuhitimisha uhusiano wa ndoa
kati ya mume na mke ulioanzishwa kwa tendo la ndoa, hivyo ni lazima uhusiano
huo uhitimishwe kwa tendo hilo kutokana na mmoja wa wanandoa kuwa amefariki.
Utakasaji huo unafanyika kwa pande zote yaani mwanake na kwa
mwanaume, lakini unatofautiana mazingira unapofanyika.
Mfano, mwanamke anapofiwa na mume wake anakodishwa mtu
maalumu wa kufanya naye tendo la ndoa na hapo kunakuwa hakuna maridhiano yoyote
kati ya mtakaswaji na mtakasaji, bali maridhiano yanatokana na kile anacholipwa
mtakasaji ndipo anafanya tendo hilo.
Lakini, mwanaume anapofiwa na mke wake anaenda mwenyewe mtaani
kutafuta mwanamke wa kufanya naye tendo la ndoa wakati mwingine akisindikizwa
na wapambe watakaothibitisha kwamba, alipata mwanamke na kufanya naye tendo la
ndoa, hivyo anakuwa ametakasika.
Wanafanya hivyo, kwa kuamini kwamba, marehemu wakati anafikwa
na mauti hakupata fursa ya mwisho ya kufanya tendo la ndoa hilo na mwenzi wake.
Kwa msingi huo, wanafanya hivyo kama
ishara ya kuhitimisha uhusiano wa wanandoa hao, yaani marehemu na yule
aliyebaki hai.
Wakerewe wanaamini kuwa, mjane au mgane akishatakaswa ile
mikosi yote iliyosababisha kifo cha marehemu inakuwa imeondolewa yote.
Pia wanafanya hivyo kwa kuamini kwamba, marehemu wakati
anafikwa na mauti hakupata fursa ya mwisho ya kufanya tendo hilo na mwenzi wake.
Hiyo inakuwa ni ishara ya kumalizika kwa uhusiano wa
wanandoa hao, yaani marehemu na yule aliyebaki hai.
UBAKAJI WENYEWE
Mmoja wa wazee anayefahamu mila hiyo ambaye pia aliwahi
kufanyiwa mila hiyo, Juma Mtallo (83) mkazi wa Nkilizi katika Kijiji cha
Mmakeke wilayani Ukerewe, anasema pindi mwanamke anapofiwa na mumewe, kama
kawaida yanafanyika matanga kwa siku kati ya tano na saba kulingana na uwezo wa
wafiwa.
Katika kipindi hicho, mjane huyo anatakiwa kuhudumiwa na
kuandaliwa chakula na mtu aliyewahi kufiwa na mwenzi wake.
“Anakuwa ndani ya nyumba amefunikwa nguo na wanaoenda
kumsalimia na kumhudumia ikiwa ni pamoja na kumpikia chakula ni wale waliowahi
kufiwa,” anasema Mtallo.
Anasema, kwa kipindi hicho anakuwa hajaoga. “Siku ya nne
ndipo wanaanza taratibu za kumuogesha na akishamaliza ndipo anapelekwa kwa
mbakaji (mtakasaji).”
Anaongeza kwamba baada ya mtakasaji kumaliza kazi hiyo,
anaondoka kwa majigambo na wakati mwingine akiimba; “Wanaume wafe wanawake
wabaki…wanaume wafe wanawake wabaki,” anasema huku akiongeza huwa anaimba hivyo
ili wanaume wazidi kufa na yeye azidi kupata kazi ya kubaka wajane.
SIKU YA UBAKAJI
Kwa mujibu wa mila hiyo, siku ya kubaka, mbakaji huwa
anaandaliwa chakula kizuri pamoja na vinywaji hasa pombe kwa gharama za familia
inayotakaswa.
Mmoja wa wanawake waliowahi kutakaswa, Anna Sebastiane mkazi
wa Tarafa ya Ukara Kata ya Bukungu, wilayani Ukerewe anasema, siku mtakasaji
anapoenda kutakasa mjane, anapokelewa kwa heshima kubwa.
Anaeleza kwamba wakati mwingine anaweza kumwambia
mtakaswaji; “Hebu cheza nione kama unaweza,”
anasema yaani aoneshe umahiri wa kutikisa nyonga wakati wa tendo la ndoa.
Anafafanua kwamba, endapo ataona mjane hawezi kutikisa
nyonga, anaongeza gharama. Mfano endapo aliwatoza fedha basi atapenda aongezewe
kiasi atakachoona kinamfaa au kama ni mifugo kama
vile mbuzi, atataka aongezewe mwingine kwa jinsi atakavyoona inafaa.
Hata pale asipovutiwa sura ya mtakaswaji, mtakasaji
anapandisha gharama kwa jinsi atakavyoona inafaa.
Anasema, endapo utakasaji utafanyika nyumbani kwa marehemu
basi ndani ya nyumba inabidi wawepo watoto wake ambao hawajaolewa.
“Wakati utakasaji unafanyika (ubakaji) watoto wanakuwa
wanasikia jinsi Omwezya (mtakasaji) anavyonguruma (akitoa maelekezo kwa sauti
nene akimwelekeza mjane jinsi anavyotaka alale au namna ambavyo anataka
atingishe nyonga yake) na hapo kitanda kinachokuwa kinatumika ni cha marehemu,”
anasema Sebastiane.
Anapoulizwa kama watoto wanasikia hiyo sauti? Sebastiane
anacheka kwanza huku akivuta pumzi, kisha anasema;
“Sio watoto peke yake, hata wanaokuwa nje wanafahamu
kinachoendelea …si unaona hali ya nyumba zetu (mbovu kiasi kwamba nyingi hazina
faragha). Anasema anakuwa anahimiza mtakaswaji atingishe nyonga ili apate raha.
“Watakasaji wengine, hawakuwa na staha na tendo la ndoa,
kwani walipokaribia mshindo (kutoa mbegu za uzazi) walipiga kelele kwa kunogewa
na uhondo wakati huo huo akiashiria kwamba kazi aliyopewa amehitimisha,”
anasema na kuongeza kuwa akishamaliza anavaa nguo na kutoka nje ya nyumba kwa
mbwe mbwe kisha kulipwa chake.
Anasema, watakasaji wengine waliondoka wakiimba; “wanaume
wafe wanawake wabaki..wanaume wa f e wa n awa k e wa b a k i . ” Anasema hiyo
kwa kufurahia kile walicholipwa. “Wakati anaondoka anapigiwa vigelegele na
akina mama kwa kufurahia kuhitimisha mila hiyo…mila hii unaweza kuiona ni
mbaya, lakini yakishakufika utaona umuhimu wake,” anasema Sebastiane.
Hata hivyo, anasema: “ Mila hii (Okusomboka) ni aibu kwa
watoto wanaokuwa ndani ya nyumba wakisikiliza mama yao akitakaswa, huku akihimizwa atingishe
nyonga… tendo la ndoa linahitaji faragha, lakini utakasaji hauna faragha na
unamdhalilisha mwanamke,” anasema na kuongeza kuwa ni jambo la aibu ndiyo maana
tendo la ndoa linahitaji faragha.
Sebastiane anapoulizwa kama mtakasaji anatumia kondomu ili kujikinga
na magonjwa, anasema jambo hilo
halipo.
Pia anasema, mtakasaji na mtakaswaji wanatakiwa wafanye
tendo moja la ndoa (yaani mshindo mmoja) na wasifanye tena tendo hilo maishani mwao,
endapo wakirudia watakuwa wamekiuka sharti la mila hiyo hivyo mikosi inaweza
kurudia familia ya mjane.
“Kwa hiyo atalazimika atakaswe (abakwe) upya na mtakasaji
mwingine, vinginevyo wanaamini kuwa familia yake itaendelea kuandamwa na
mikosi,” anasema .
Anataja mikosi hiyo kuwa ni pamoja na familia kuandamwa na
vifo na kuugua mara kwa mara.
MASHAHIDI
Mashahidi wanaoshuhudia tukio hilo,
wanasema wanakuwepo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tendo hilo limefanyika, ili kuondoa wasiwasi wa
wajane kudanganya.
Mjane mwingine, Arodia Gabaseki (64) mkazi wa Kata ya
Ulagala, Tarafa ya Masonga wilayani Ukerewe anasema mashuhuda wanakuwa nje
katika mazingira ambayo watakuwa na uhakika kuwa tendo hilo linafanyika.
Anasema kwamba, kutokana na wajane kuogopa mikosi, lazima
wakubali na kwamba mgurumo wa mtakasaji nao kwa wakati mwingine ni ishara nzuri
kwao.
Anaeleza kwamba, mara baada ya kutakaswa anarejea nyumbani
akiwa ameinamisha kichwa chini na kupokewa kwa furaha na wanandugu waliopo
kwenye matanga, kwa kuwa wanaamini kuwa uhusiano kati ya mjane na marehemu
umehitimishwa na hakuna matatizo yoyote yanayoweza kuwapata.
SIFA YA MTAKASAJI
Ofisa wa Taasisi ya Kuboresha Mila na Desturi katika Jamii
ya Ukerewe (KUMIDEU), taasisi ambayo inajihusisha kutoa elimu ya kutokomeza
mila ya kutakasa wajane, Musiba Kakulu anasema mtakasaji ni mtu anayeonekana
hakubaliki ndani ya jamii kutokana na matendo hayo.
Anasema, watakasaji wengi ni walevi, wachafu, wasiokuwa na
wanawake na mara nyingi walitegemea kuendesha maisha yao kwa kutegemea malipo wanayopata kwa njia
ya utakasaji.
“Kutokana na umuhimu wa mila ya kutakasa, mtakasaji
(Omwezya) anakuwa hana umuhimu ndani ya jamii,” anasema Kakulu. Sifa nyingine
anasema ni mtu anayejua dawa na anayependa kusimamia mila na desturi.
Pamoja na kuwa na hali hiyo, lakini thamani yao inaonekana pale walipohitajika kutakasa,
kwani watu wenye heshima zao ndani ya jamii hawakubali kabisa kutakasa watu
ambao tena haijulikani wenzi wao wamefariki kwa magonjwa gani.
“Mtakaswaji kama ni bibi kikongwe, anapata shida kwani
mtakasaji anatoza gharama kubwa kama vile
ng’ombe wakati uwezo anakuwa hana, lakini ndugu lazima wachangishane ili
wampate ng’ombe huyo,” anasema.
Anasema, wakati mwingine
mtakasaji anapotakiwa kwenda kwa mtakaswaji na ni mzee sana analazimika atafutiwe usafiri hadi
nyumbani kwa mjan