- AFICHUA SIRI NZITO KUHUSU UBUNGE WAKE
Na Anneth Kagenda KWA HISANI YA MAJIRA
MBUNGE
wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), ame s ema h a f i k i r i I kugombea
urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.Alisema
mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta
chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasiliBw.
Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku
chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya
wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015. Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi
ya pili katika mchujo huo
ambapo
Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na
Teknolojia,
Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM)
Mwanasiasa
aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam,
Bw.
John Mnyika (CHADEMA),"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na
siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama
nitakosa ni bora nikalime michikichi...sihitaji urais," alisema.
Katika
mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa
nchi kamaatagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi
sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani. Wanafunzi hao
walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na
vurugu,
kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa
tindikali na
kupungua
kwa mtangamano wa kijamii. Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani
Morogoro
ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi
ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw.
Kabwe alipata kura 20.Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe
kijana mwenye fi kra mpya, atakayeleta matumaini mapya,
kuwaunganisha
Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila. Sifa nyingine ni
kiongoz mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo
viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake