Kuna baadhi ya vipande havikurekodiwa kutokana na mambo yaliyotokea wakati wa kuandaa hii video mfano ukiangalia kwa makini, kuna scene ya upande mmoja tu ambapo Jokate anaonekana kumuonea wivu Lucci akiwa na msichana mwingine wakati wimbo unasema pia Lucci anajua Jokate ana boyfriend na ana wivu juu ya hilo.
Plan za video ilitakiwa kuwe na scene ikimuonyesha Lucci anamuonea wivu Jokate, lakini haikuweza kurekodiwa.
Unaambiwa kuna baadhi ya scene hazikuwekwa kwenye video ambazo Jokate alikuwa anacheza, scene hii ilifanyika usiku sana na Jokate alikuwa amechoka, producer akaamua wasiziweke kwenye video kwasababu hakuchangamka kama walivyotegemea.
Kauli ya Lucci ni kwamba kuna mambo mengi ambayo ni mazuri kuona hasa kutokana na ukali wa video yenyewe ndio maana wameamua kuitengenezea documentary, endelea kupita hapa millardayo.com kwa ajili ya info zaidiobama