Wafanyabishara ndogo ndogo katika mitaa ya Juba, South Sudan (2012 photo) Serikali ya Jubaland imewafukuza wafanyabiashara katika mitaa ya Halanle na En-Arga na kudai eneo hilo litatumika kama kituo cha jeshi ili kuweza kuimarisha usalama katika eneo.
Wafanyabiashara katika mitaa hiyo wamelaani kitendo hicho wakisema kuwa serikali imewakoseshwa kipato ambacho walikuwa wakiingiza kwa siku na kuweza kujikimu kimaisha pamoja na familia zao.
Akizungumza na Sauti ya America mwandishi wa habari Ahmed Ali Ahmed anasema wafanyabiashara hao wanadai kwamba kwa kawaida bidhaa wanazoziuza huwaingizia kipato cha kati ya shilingi 400,000 hadi 500,000 za Somalia ambazo ni sawa na dola 20 hadi 25 ya Marekani. Kiwango hicho huweza kuwasaidia kulipa bili za nyumbani na kiasi kingine hata kuhifadhi kwenye akaunti zao katika benki.