wakaguzi wa silaha za kemikali wa Umoja wa Mataifa mjini Damascus Aug.26, 2013
a wamechukua sampuli za damu kutoka kwa waathiriwa wa shambulizi la kemikali la wiki jana lililofanywa na wanajeshi wa Syria.Timu hiyo ya Umoja wa Mataifa ilitembelea mojawapo ya vitongoji vya Damascus ambapo waasi wanadai kuwa serikali ilitumia gesi ya sumu na kuuwa mamia ya raia. Lakini timu hiyo pia ililengwa kwa mashambulizi yaliyoharibu gari lao na kuwafanya wakaguzi hao kurudi nyuma.
hakileoNaye waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema ni jambo lisilofichika kuwa silaha za kemikali zilitumika nchini Syria na kuiita hatua hiyouovu wa kimaadili.
Akizungumza katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani Jumatatu,Kerry alisema rais Barack Obama anaamini lazima kuwe na uwajibikaji kwa wale wanaotumia silaha za aina hiyo ingawa hakusema rais huenda akachukua hatua gani.
Msemaji wa White House Jay Carney alisema Jumatatu kuwa rais Obama anatathmini jibu sahihi na kwamba hajafikia maamuzi ya hatua atakayochukua. Lakini akaongeza kuwa hapana shaka serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali.
Wakati huo, huo rais wa Marekani Barack Obama anatafakari juu ya swala la kushambulia Syria kutokana na ripoti kwamba ilitumia silaha za kemikali dhidi ya wapinzani wake lakini ni sharti afanye tathmini kubwa ya kisheria juu ya hatua hiyo.
Katiba ya Marekani inatambua rais ndiye kamanda mkuu wa majeshi lakini pia inatoa mamlaka kwa bunge kutangaza vita na kudhibiti fedha zitakazotumiwa katika vita kama hivyo.
Pamoja na hayo sheria za miaka 40 za Marekani juu ya vita zinamlazimu rais kufahamisha bunge katika muda wa saa 48 baada ya kuamua kuchukua hatua ya kijeshi na inaweka marufuku kwa majeshi kubaki vitani kwa zaidi ya siku 60 bila idhini ya bunge.