RAIS Paul Kagame wa Rwanda, sasa hayupo tayari kukanyaga ardhi ya Tanzania kutokana na kile kinachoonekana kuwa ni mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea kati yake na Rais Jakaya Kikwete. MTANZANIA Jumatano limedokezwa.
Wakati hayo yakifikia hapo, kikao cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA), linakoketi mjini Arusha kilivunjika baada ya Spika wa bunge hilo, Magreth Zziwa, kugongana kauli na Mbunge mmoja wa Rwanda jambo lililosababisha wabunge wote wa Rwanda kususia kikao na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.
Mwenendo wa hayo yaliyojitokeza jana katika Bunge la Afrika Mashariki hadi kikao kuvunjika, msingi wake ni mgogoro unaowagusa wakuu hao wawili wa dola.
Habari zilizolifikia gazeti hili toka katika vyanzo vyake mbalimbali vilivyo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, lakini pia katika vikao vya Bunge hilo la Afrika Mashariki vinavyoendelea jijini Arusha zinaeleza kuwa, Rais Kagame hata kama ataalikwa kuja nchini leo, hatakuja.
www.hakileo.blogspot.com
MTANZANIA Jumatano limedokezwa kuwa jambo hilo tayari limethibitishwa na Wabunge wa Rwanda wanaohudhuria vikao vya (EALA).
Taarifa toka ndani ya Bunge hilo zilizolifikia MTANZANIA Jumatano zinaeleza kuwa, tayari mzimu wa msigano huo uliojitokeza baina ya wakuu hao wawili wa dola, umeanza kuwavuruga wabunge hao baada ya jana kikao cha Bunge hilo kuvunjika, kutokana na kuibuliwa kwa hoja ya kutaka vikao vya Bunge hilo kufanyika kwa utaratibu wa kuzunguka kila nchi.
Zinaeleza zaidi kuwa; Ni katika hoja hiyo wabunge wa Kenya na Rwanda walionekana kuungana na kuwa kitu kimoja na hivyo kususia kikao hicho cha jana, jambo ambalo lilimlazimisha Spika wa Bunge hilo, Magreth Zziwa kuvunja kikao