MADIWANI BUKOBA SASA KICHEKO
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM), imetoa maamuzi juu ya
sakata la madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri kuu
ya chama hicho mkoani Kagera hivi karibuni.
Katika maamuzi yake,
Kamati Ku u ime b a t i l i s h a u amu z i uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM,
mkoani humo Agosti 13 mwaka huu wa kuwafukuza uanachama madiwani haoKutokana na maamuzi hayo, madiwani hao
ni wanachama halali wa chama hicho.Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya
habari na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, ilisema
Kamati Kuu imetoa uamuzi huo baada ya kubaini kuwa, Halmashauri Kuu ya CCM,
mkoani humo haikuzingatia katiba ya chama ya 1977,toleo la 2012 Ibara ya 93
(15).
Ibara hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi
ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi
yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya
Mkoa, isipokuwa suala la kumvua uanachama au uongozi diwani, lisifanyike hadi
Kamati Kuu imearifiwa na kutoa maelekezo.
Kamati Kuu imewaonya madiwani wa CCM
Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki na Meya wa
Manispaa ya Bukoma Mjini, Dkt. Anatory Amani kwa kusababisha kukosekana utulivu,
mshikamano na amani katika manispaa na ndani ya chama.
Pia kamati hiyo imeitaka Serikali
kumwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi
maalumu juu ya mambo yanayolalamikiwa dhidi ya Dkt. Amani ili ukweli uweze kujulikana
na matokeo ya uchunguzi huo yawasilishwe kwenye Baraza la Madiwani ili hatua
stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za
Mitaa.
Wakati tuhuma hizo dhidi ya Meya zikichunguzwa, Kamati Kuu imewataka
madiwani hao kurejesha utulivu kwenye manispaa na chama ili kufanikisha
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi wa
Bukoba. fukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya chama hicho, mkoani Kagera,
hivi karibun www.hakileo.blogspot.com