Na Livinus Feruzi, Bukoba
MATENGENEZO ya
uboreshaji njia kuu za kusafirisha umeme yanayotarajiwa kufanywa na Shirika la
Umeme nchini (TANESCO), kutoka Masaka nchini Uganda hadi Mutukula nchini
Tanzania, yatasababisha Wilaya tatu za Mkoa wa Kagera kukosa huduma ya umeme
kwa wiki 40.
Wilaya
ambazo zitaathirika na uboreshaji huo ni pamoja na Bukoba, Muleba na Karagwe,
ambapo Meneja wa TANESCO, mkoani humo, Martin Madulu, alisema zaidi ya kilomita
1,000 za njia ya umeme zitafanyiwa ukarabati.Alisema
matengenezo hayo yataanza Septemba mosi mwaka huu na yatafanyika kwa siku tatu
kila wiki kwa majuma 40.
"Umeme
utakuwa ukikatwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kuanzia asubuhi hadi
jioni... hali hii inatokana na uchakavu wa miundombinu ya kusafirisha umeme
kutoka maeneo husika."Viongozi
wa pande zote (Uganda na Tanzania), wamekubaliana kufanya ukarabati huu ili
kuboresha huduma...mapendekezo ya viongozi wa Uganda walitaka umeme ukatwe wiki
nzima ili matengenezo haya yachukue miezi mitano," alisema.
Aliongeza kuwa, pendekezo hilo halikukubaliwa baada ya kubainika kuwa,
madhara yangekuwa makubwa miongoni mwa jamii. Aliwaomba wananchi kuwa
wavumilivu kwa muda wote wa matengenezo hayo