Umoja wa Mataifa umesema kwamba mmoja wa askari wake ameuwawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia mapigano makali na waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Msemaji wa Shirika hilo mjini New York, Farhan Haq, hakufichua mwanajeshi huyo ni wa taifa lipi na pia alikataa kutoa taarifa zozote kuhusu wanajeshi waliojeruhiwa.
Majeshi ya Umoja wa Matiafa walitumia helikopta kuwasukuma nyuma wapiganaji wa M23 kutoka maeneo ambayo wamekuwa wakiyashikilia katika mji wa Goma.
Katika mapigano yalitokea wiki iliyopita watu zaidi ya 80 waliripotiwa kuuwawa.
Waasi wa M23 waliuteka mji wa Goma mwaka 2012 lakini walilazimika kujiondoa kufuatia shinikizo kutoka jamii ya kimataifa.
Wakati huu Umoja wa mataifa umetuma kikosi maalum ilikutatua tatizo la uasi katika taifa hilo la Congo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Waasi wa M23 wanadai kuwa jeshi la Congo likisaidiwa na kikosi maalum cha www.hakileo.blogspot.comumoja wa mataifa lilishambulia mji wa Goma kutoka angani na kwa kutumia silaha nzito nzito.
Wapiganaji wa M23 ni mkusanyiko wa watoro toka jeshi la kitaifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Na hadi wakati huu karibu watu 800,000 wametoroka makaazi yao tangu waasi waansihe harakati zao.