AJTC STAR NA TASWA DAR NJIA PANDA, pia ona picha za Media Bonanza.

HABARI ZETU
Hiki ndicho kikosi cha AJTC STAR
Hiki ndicho kikosi cha TASWA DAR kilicho na  waandishi mahiri wa habari za michezo.
Wachezaji wa timu ya AJTC STAR wakipiga na vilivyo uwanjani.
Katika hali ya kushangaza iliyotokana na uzembe timu ya chuo cha uandishi wa habari Arusha AJTC, ili lazimika kumpata bingwa pacha ambae ni timu ya TASWA kutoka Dar es salaam kwenye fainal ya mpira wa miguu .

Kutokana na muda kumalizika timu hizo zikiwa zimetosha na nguvu ndipo walilazimika kupigiana matuta huku timu zote zikiwa zime piga matuta mawili mawili na kila timu kukosa moja, waamuzi wa mpambano huo walilazimika kuukatisha kwani giza lilitanda haliiliyo wafanya wapigaji na walinda milango kushindwa kuona vizuri.
Wakwanza kulia ni waziri wa michezo chuoni hapo George Samba akiwa na mashabiki wa timu yake wakati wakijiandaa kwenda kiwanjani.

Waandaji wa shindano hilo la bonanza ambao ni TASWA  ya mkoa wa Arusha waliamua ya kwamba washindi wa gawane zawadi ambapo kila mmoja aliambulia shilingi laki mbili mbili fedha tasilimu.Huku kikombe kikibaki kwenye stoo ya wandaji hao paka pale mechi ya kutafuta mshindi itakapo pigwa.


Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa siku isio julikana kwenye mkoa wa Dar es salaamu, lakini mwalimu wa nmichezo wa Chuo cha AJTC Luckas Modaha amekaririwa na meza yetu akibeza mpango huo kwani kwake ni kama danganya toto kwa madai kwamba kama zawadi zenyewe ni finyu watawezaje kuisafirisha timu.
"sasa kama zawadi zenyewe ni laki mbili  kwa mshindi iweje waweze kutusafirisha hadi Dar , nakutulipia malazi ..ni jambo ambalo hali wezekani" alisema mwalimu huyo alie kuwa akishangiliwa na wanafunzi wake katika ukumbi wa chuo hicho.

Timu ya taswa ya Dar ilisheheni waandishi mahiri wa habari za michezo kama vile Shafii Dauda na wengineo,ikumbukwe kwamba chuo cha AJTC ndio waliokuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo kwa upande wa mpira wa miguu.

Yote katika yote wandaji wa michuano hii hawata kwepa lawama kwani kitendo cha fainali kuchezwa dakika ishirini yaani kumi kipindi cha kwanza na kumi kingine sii cha kimichezo na baya zaidi muda kuto kutosha.
Bonanza hilo lilifanyika kwenye viwanja vya General Trire vilivyopo Njiro Mkoani Arusha na kuhusisha vyombo mbali mbali vya habari ikiwemo Arusha One,Radio Five na ORS pia Sunrise Radio.www.hakileo.blogspot.com
Kama kawaida mashabiki nao hawakusalia nyuma,  anaonekana kulia ni Gundelinda Kiumbi shabiki wa AJTC STAR

 KATIKA MCHEZO WA KWANZA TIMU YA AJTC STAR ILIFUNGWA NA ARUSHA ONE KWA MAGOLI 2-1 HUKU GOLI LA PILI LIKIZUA UTATA NA MARA BAADA YA MCHEZO KOCHA WA AJTC STAR ALIMVAA MWA MUZI.
Hatimae walifanikiwa kutuliza hasira zake
                                                        ONA PICHA HAPA.
Wakwanza kulia ni naodha watimu hiyo akijaribu kupunguza hasira za kocha wake Charles Dida baada ya kumvaa mwa muzi kwa madai ya upendelea na kumtukanaa,wengine ni wanakati wa michezo choni hapo, kushoto akiwa ni Iddi Abdalah na wapili kushoto ni Nassoro Muhemed.
Huyu ndie mwamuzi aliezua utata na hatimae kumtukana kocha wa AJTC STAR.
                                       
Pilau nalo haliku pigwa chenga kwani maandalizi yake wachezaji na wanaamati waliandalia msosi wa nguvu.

Na hili ni miongoni mwa magari yalio wapeleka mashabiki na wachezaji wa AJTC STAR kwenye Bonanza hilo.



Wanasema kazi na sala na hapa wanaswali kabla ya mchezo wao wa ufunguzi na Timu ya Arusha one.

Haw ndio waamuzi waliochezesha michezo yote.


Ujumbe wa bonanza haukubaki nyuma ila hapa wamesahau kutuambia ni bonanza la ngapi kuna ujumbe na wadu wa habari mkoa wa Arusha ila timu kutoka Dar zilishiriki.

Vikosi vyote viwili vya AJTC na Arusha One vikijianda kujimwaga dimbani.




Bado haliiliendelea kuwa tata.

Ilimlazimu shabiki kiani kuingia uwanjani na kuongeza nguvu.

Alitamani kurudi tena ila walindhiti vilivyo.





Hili ndilo jukwaa la mashabiki na wageni walikwa.


Mashabiki wa AJTC STAR wakishabikia timu yao.

Mashindano ya kufukuza kuku hayaku salia nyuma na huyu ni mfulkuza kuku kutoka timu ya TASWA DAR.
Sara Peter ndie ali ibuka kidedea kwa upande wa kundi lake na hapa na piga jaramba.
Mambo yaliwivaa mara baada ya kipenga kilicho waruhusu kuanza kutimua mbio na kitoweo.



Mara baada ya ushindi ndimpozi zilionesha furaha yake.

Nao Arusha One hawaku salia nyuma kwani Paselina Mshana aliibuka wa kwanza kwenye mbio kwenye kundi lake na hatmai kumnyakua kuku.

Haukua ushuindi wake tuu bali wa redio nzima kwani alie katikani ndie meneja wa kituo hicho Hamisi Mpinga na wa kwanza kulia ni mtoto wa mmiliki wa kituo hicho.

Wakwanza kulia mbele ni mkurugenzi wa mafunzo wa chuo cha AJTC JOSEPH MAYAGILA na  wakanza kushoto ni mkufunzi wa chuo hicho IZACK CHIWANGA,walioko nyuma yao ni wachezaji wa timu yao wakipiga jaramba.

Huyu ni golikipa wa timu ya Sunrise akijianda na kukabiliana na mikwaju ya penati ambapo timu yake ilitolewa kwenye hatua hiyo.

Mchezaji wa timu ya AJTC STAR akiwa amebebwa na mc
hezaji mwenzake mara baada ya kuwezesha timu yake kutinga fainali kwa kufunga mkwaju wa misho wa penaliti.
Aliebebwa ni golikipa wa timu ya AJTC STAR Kelvin alimarufu kama Masta akiwa amebebwa na mchezaji mwenzake aitwae Jere baada ya kuiwezesha timu yake kutinga fainali kwa kupangua mikwaju kaadhaa ya penaliti..

Burudani ya muziki nayo haikutelekezwa na hapa ni bendi malumu ikitoa raha kwa wanabonanza.

Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company