Usingizi unasaidia kukuza celi za ubongo wako
Wanasayansi wanaamini kuwa wamepata sababu moja mpya ya kwa nini tunahitaji usingizi.
Wanasema kuwa kulala kunasaidia katika kujenga celi mpya za ubongo.
Matokeo ya utafiti huu ambayo yalijitokeza katika panya wa mahabara, huenda yakachochea maelezo zaidi kuhusu umuhimu wa usingizi katika kukabarabati celi za ubongo na kukuza celi mpya pamoja na kuulinda kutokana na magonjwa.Usingizi unasaidia kuzalisha upya celi za ubongo ambazo nazo hujenga kemikali inayojulikana kama Myelin ambayo ni muhimu katika kulinda ubongo wetu kwa ambavyo unafanya kazi.
Daktari
Chiara Cirelli na wenzake kutoka chuo kikuu cha Wisconsin waligundua
kuwa Panya hao walipokuwa wanalala, ndipo kemilaki hiyo ilikuwa
inatengezwa kwa wingi na celi za mwili.
Ongezeko la kemikali pia ilitegemea aina ya usingizi ambao Panya walilala hasa uliohusishwa na ndoto.
Kinyume na hilo, celi zilionekana kufariki wakati Panya walipokuwa wako macho wazi.
Na
hii ndio maana usingizi ni muhimu jambo ambalo wamekuwa wakilihoji
wanasayansi kwa miaka mingi. Yaani nini umuhimu wa usingizi?
Ni
wazi kuwa tunahitaji kulala ili kupumzika na ili ubongo wetu ufanye
kazi vyema....lakini mambo ya kibayolojia yanayofanyika tunapokuwa
tumelala ndio yameanza tu kugunduliwa.
Daktari
Cirelli alisema kuwa : "kwa muda mrefu, watafiti wa usingizi wamekuwa
wakilenga tofauti iliyopo kati ya celi za neva wakati wanyama wanakuwa
hawajalala na wakti wamelala. Kwa sasa ni bayana kuwa celi zengine
kwenye mfumo wa neva hubadilika kutokana na usingizi.''
Watafiti
hao wanasema kuwa matokeo yao yanapendekeza kuwa ukosefu wa
usingizi,unaweza kusababisha maradhi ya ubongo yanayoathiri celi zake.
Watafiti
hao pia wanataka kuchunguza ikiwa vijana kukosa usingizi wakati
wanapokuwa huenda ikaathiri ubongo wao katika siku za usoni.
Usingizi ni muhimu kwa mfumo wa neva mwilini ili uweze kufanya kazi vyema.
Usingizi pia husaidia katika uzalishaji wa homoni zinazowafanya watoto na vijana kukuwa.
