Mabomu yaripua hoteli mbili Mogadishu

HABARI ZETU
Polisi nchini Somalia wanasema mashambulio mawili ya mabomu mjini Mogadishu yameuwa watu kama 15.
Polisi walieleza kuwa mabomu hayo yaliripuka kwenye mkahawa uitwao The Village ambao unapendwa na waandishi wa habari na maafisa wa vikosi vya usalama, pamoja na hoteli Muna, ambako wabunge wengi hukaa.
Hoteli zote mbili ziko karibu na ikulu ya rais.
Hakuna aliyedai kuhusika na mashambulio hayo, lakini hoteli zote mbili zimewahi kushambuliwa na wapiganaji wa Kiislamu, al Shabab
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company