HABARI ZETU
.bmp)
Huyu ndie mkurugenzi wa chuo cha AJTC kilichopo mkoani Arusha eneo la Kwa Morombo,anaitwa Joseph Mayagila.
Mkurugenzi wa mafunzo wa chuo cha uandishi wa habari na utngazajiwww.hakileo.blogspot.com Aarusha Jeseph Mayagila alimarufu kama Prosesa Josee amehaidi kuliteka soko la uandishi wa habari nchini Tanzania.
Akizungumza mapema leo aluudhri katika ukumbu wa chuo hicho mkurugenzi huyo amehaidi kuhakikisha ya kwamba miaka michache ijayo nusu ya waandishi na watangazaji watanzania watatoka katika chuo hicho.
Pro fee Josee ameyanena haya wakati akizundua bonanza la mashindano ya utangazzaji
yanayo wahusisha wanafunzi wa chuo hicho huku mchuano makali ukiwa ni kati ya wanafunzi wa ngazi ya cheti na stashahada.
Michuano hiyo inatarajiwa kumalizika ijumaa ijayo huku washindi wakihaidiwa zawadi kemu kemu,pia mkurugenzi huyo amehaidi kuwapeleka “out” wanafunzi ambao darasa lao litafanya vizuru zaidi.
Madarasa kadhaa leo yanatarajiwa kuchuana ikiwemo darasa la Tanganyika,Mkomanzi na Tarangire.Kwa siku ya leo kipengele kitakacho anza ni kile cha Vipindi maalumu huku vinginevyo kama vile Tarifa ya habari na michezo vikiendelea hadi alihamisi ambapo ijumaa ndiyo fainali.
Kwanzia leo hadi hiyo alihamisi majaji watakuwa ni wakufunzi wa chuo hicho huku siku ya fainali wakitarajia kuwa na jaji kiongoizi ataetoka nje ya chuo hicho ambae anatarajiwa kuwa ni mwandishi wa habari au mhariri.
Kwa upande wake mkurugenzi huyo amewatoa hofu washiriki wake ya kuhusau hujuma au uchakachuaji kwani ana waamini majaji wake.
“wasiwe na hofu kwani majaji wetu tumewaandaa vizuri na hawata kuwa na upendeleo wowote kwani ni waadilifu”Amesisitiza mkurugenzi huyu.
Ila kwa siku ya leo wakufunzi wa chuo hicho ndio waliofungua dimba kwa kuendesha baadhi ya vipindi ikiwemo Elifuraha Samboto aliesoma taarifa ya habari na michezo huku Luckasi Modaha akiendesha matukio.
Pia madamu Verediana Akonai ameendesha kipindi malumu wakati huu madamu Neema anaendesha kipindi cha Watoto katika studio za redio za chuo hicho.