Rwanda yaongeza ushuru wa mpakani na Tanzania kwa zaidi ya asilimia 200.

Rais wa Rwanda  Paul Kagame.www.hakileo.blogspot.com

Rais wa Rwanda Paul KagameRwanda imeamua kupandisha ushuru wa magari ya mizigo kutoka dola za Marekani 152 hadi 500 kuanzia tarehe 9 Septemba mwaka huu.
Akizungumza na Sauti ya Amerika waziri wa miundo mbinu wa Rwanda Bw. Silas Gwakabamba alisema ushuru huo mpya ambao ulisababisha mtafaruku katika eneo la Rusumo umesitishwa kwa muda kwa muda ili kuruhusu wafanyabiashara waliokuwa wamekwama mpakani humo kuweza kuendelea na safari zao.
Iliripotiwa kuwa  magari yapatayo 200  ya mizigo yalikwama katika eneo la Rusumo mpakani mwa Rwanda na Tanzania baada ya kutangaziwa kodi hiyo mpya , akifafanua hali hiyo waziri huyo wa miundo mbinu wa Rwanda amesema magari hayo yameachiwa kwa sasa.

Waziri ameongeza kumekuwa na mazungumzo kati ya mawaziri wa fedha wa nchi hizo na bei hiyo iliamuliwa na Rwanda kwasababu wao pia walikuwa wakilipishwa dola hizo 500 wakielekea Tanzania, lakini aliongeza anavyoelewa mawaziri walijaribu kukubaliana juu ya msingi wa mahesabu na waziri wao wa fedha ndiye anashughulikia suala hilo.

Na anaamini kuna makubaliano yanayoendelea  kati ya serikali hizo ambapo kwa upande wa Mombasa na Kampala tayari wamekubali kuondoa vikwazo vingi barabarani ila upande wa Tanzania bado akiongeza kuwa waziri wa Tanzania tayari ameshafika Rwanda mara mbili kuongelea suala hilo
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company