Magavana wa Benki ya dunia na IMF wana wasiwasi na athari zinazotokana na kudorora kwa uchumi wa dunia


Magavana wa Benki ya dunia na shirika la fedha la kimatiaf IMF kutoka Afrika wamesema wana wasiwasi na ongezeko la athari zinazotokana na kudorora kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika.

Kwenye taarifa yao, magavana hao wamesema athari hizo zimeendelea kuongezeka barani Afrika licha ya pengo la bajeti, kupungua kwa bei za bidhaa, kupungua kwa biashara na ukosefu wa mikopo nafuu. Kwa mujibu wa ripoti ya IMF na World Bank, uchumi wa dunia unatarajiwa kukua kwa asilimia 2.9 mwaka huu ikiwa ni chini kwa asilimia 0.3 iliyokaridiriwa mwezi Julai mwaka huu. Magavana hao pia wameonyesha wasiwasi wao kuhusu sera hafifu za fedha na tishio la changamoto za bajeti ya Marekani ambalo kama halitashughulikiwa huenda likahujumu juhudi za ukuaji. Magavana hao pia wamesema watunga sera wa nchi zilizoendelea wanatakiwa kutambua matokeo mabaya ya sera zao na kuhakikisha kuwa mipango yao ya kuondokana na msukosuko wa fedha inafaa kuelezwa waziwazi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company