Seleka wavishambulia vikosi vya CAR



Waasi wa zamani wa muungano wa Seleka wameanzisha amshambulizi dhidi ya vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati vilivyotumwa kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, kufuatia mapigano ya hivi karibuni yaliyopelekea watu 50 kuuawa. Mashambulizi hayo yaliyowajeruhi raia wawili yalijiri juzi katika kijiji cha Garga umbali wa kilomita 200 kaskazini magharibi mwa Bangui mji mkuu wa nchi hiyo. Kanali Christian Djouma Narkoyo wa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati ameeleza kuwa ni waasi wa zamani wa muungano wa Seleka ndio waliotekeleza mashambulizi hayo. Amesema ni jambo linalovunja moyo kuona wapiganaji hao wa zamani wakitekeleza mashambulizi kama hayo. Kanali Narkoyo amesema hatua zitachukuliwa ili kukomesha hatua hizo za waasi wa zamani wa muungano wa Seleka.

Jumanne iliyopita watu 50 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mapigano yaliyojiri kati ya waasi wa zamani wa muungano wa Seleka na makundi mengine ya wanamgambo yanayobeba silaha huko katika eneo la Garga umbali wa kilomita 200 kutoka mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company