Picha aliyo-tweet Hans-Christian Stroebele akiwa na Edward Snowden (L) mahali fulani huko Moscow, Urusi, Oktoba 31, 2013.
Aliyekuwa mwajiriwa wa Wakala wa Serikali wa Usalama wa Taifa la Marekani (NSA) nchini Marekani amepata kazi ya kusimamia tovuti, ambayo kama ilivyo usiri wa sehemu anayoishi huko Urusi, vile vile jina la tovuti hiyo nalo halijawekwa bayana.
Picha inayoonekana hapo inamwonesha Snowden akiwa na mmoja wa watunga sheria wa Ujerumani, na mwanakamati wa Kamati ya Bunge inayohusika na uangalizi wa shughuli za Mashirika ya Kiusalama ya nchi Ujerumani, Hans-Christian Sroebele ambaye walionana hivi karibuni kwa lengo la kuzungumzia zaidi kuhusu shughulli za udukuzi za NSA
Barua aliyoiandika kwa anwani ya Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel akiielekeza kwa Serikali ya Ujerumani, alimkabidhi
mmoja wa watunga sheria wa Ujerumani, Hans-Christian Sroebele, ambaye naye aliiwasilisha kwa wanahabari Ijumaa ya leo, amesema kusema ukweli kamwe si kosa na hivyo anaamini uungwaji mkono anaoupata baada ya kufichua siri na shughuli za NSA, zitasaidia kuishinikiza Serikali ya Marekani kupunguza 'tabia haribifu' ambayo inamzuia pia kutoa siri zaidi za udukuzi unaofanywa na Serikali hiyo.
Snowden amekaririwa pia akisema kuwa yupo tayari kwenda nchini Ujerumani kusaidia uchunguzi kuhusia na na udukuzi unaodaiwa kufanywa na Marekani dhidi ya Kansela Merkel.
Wakati huo huo, kitengo cha Haki na Sheria cha Serikali ya Marekani kimejiunga kwenye kesi iliyofunguliwa dhidi ya 'mvunja jungu' (whistle-blower) aliyeishitaki shirika la USIS (United States Investigations Services) iliyopewa dhamana na mkataba tangu mwaka 1996 kwa ajili ya usalii na usajili wa watu wanaoomba kuajiriwa wa Serikali, kuwa haikufanya kazi yake kwa makini katika kuchunguza nyendo za nyuma za Snowden (quality control reviews in background check) na hivyo kushindwa kumshauri vyema mwajiriwa wake. Mashitaka hayo yalifunguliwa katika mahakama ya Alabama zaidi ya miaka miwili iliyopita.
USIS ndiyo iliyohusika pia na kuajiriwa kwa Aaron Alexis, askari mtaalamu wa teknolojia, aliyefyatua risasi katika ofisi za kituo cha jeshi la maji na kuua watu 12 huko Washington mwezi uliopita.
Tayari msemaji wa USIS amekiri kuwa wanashirikiana na Serikali katika uchunguzi na tayari wameshafanya marakebisho ya kiuongozi ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika kazi zake tangu mwaka jana zilipoanza kutoka kashifa dhidi yake.
USIS inashutumiwa kuzembea na kufanya kazi yake kwa kulipua kuanzia mwaka 2008 ili kufikia malengo ya Serikali.
Source: www.wavuti.com