MFANYABIASHARA Musa Boazi (19), mkazi wa Kisukuru-Ukonga, amekufa kwa kujinyonga na kamba ya manila.
Boazi alikutwa amekufa juzi, saa 8 mchana maeneo ya nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema kuwa maiti ya mtu huyo ilikutwa ikining’inia nyuma ya mlango wa choo cha nyumba aliyokuwa akiiishi.
Alisema sababu za kujinyonga hazijafahamika, kwa kuwa marehemu hakuacha ujumbe wowote. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wakati huohuo, mwanaume mlemavu asiyefahamika amekutwa amefarika maeneo ya Kurasini Biashara Club-Chang’ombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiongo, alisema maiti ya mtu huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 40-45 ilikutwa ikiwa imelala katika kibanda cha madereva teksi huku ukiwa hauna majeraha yoyote huku baiskeli yake ya miguu mitatu ikiwa pembeni. Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Temeke.
Wakati huohuo, juzi zimekutwa maiti za watoto wawili wa kike na kiume wenye umri wa siku moja zikiwa ndani ya boksi zimetupwa na watu wasiofahamika maeneo ya Kigogo Dampo.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago