TIDO AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI


Mama mzazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando, Jessie (85), amefariki dunia Chang'ombe jijini Dar es Salaam kwa ugonjwa wa moyo.

Akizungumza jana jioni, Tido alisema mama yake ( alifariki baada ya hali kubadilika ghafla).

"Alikuwa na matatizo ya moyo kwa siku nyingi, lakini hali ilibadilika ghafla, akafariki akiwa nyumbani," alisema.
Tido alisema taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Chang'ombe, karibu na Klabu ya Sigara. "Tunafanya maandalizi, taratibu zinasubiri watoto wa marehemu waliopo Uingereza, Marekani na Australia, mwili utasafirishwa Tanga kwa maziko."

Ameacha watoto wanane, enzi ya uhai wake alifundisha Shule za Msingi Mgulani, Kibasila za Dar es Salaam. Nyingine ni katika mikoa ya Tanga, Dodoma, Morogoro, Iringa, Arusha na Mwanza.CHANZO MWANANCHI
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company