CHRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA FIFA BALLON D'OR 2013



MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ameuvunja utawala wa miaka minne wa Lionel Messi wa Argentina anayechezea klabu pinzani ya Barcelona baada ya kunyakua tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Fifa usiku wa kuamkia leo.Ronaldo amemshinda pia Franck Rivery, Mfaransa anayechezea Bayern Munich.

Sherehe za tuzo hizo zilifanyika Zurich, Uswisi.



Nadine Angerer

Kwa upande wa wanawake, kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani, Nadine Angerer ameibuka kinara mbele ya Marta (Brazil) na Abby Wambach (Marekani). Mdada huyo aliisaidia Ujerumani kutwaa taji ya Euro 2013 kwa wanawake akiokoa penati katika mechi yao ya fainali dhidi ya Norway waliyoshinda 1-0
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company