Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Iran
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-moon ameikaribisha Iran katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa amani kuhusu Syria utakaofanyika wiki hii, hatua iliyousababisha upinzani mkuu kutishia kuususia mkutano huo.
Muungano wa kiatifa wa upinzani Syria, unapinga kuhusuika kwa Iran, lakini Ban ki Moon anasema anaamini kwamba Iran inapaswa kuwa sehemu ya suluhu ya mzozo huo.
Katika mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa alituma mwalikio huo kwa serikali ya Iran, baada ya kushauriana kwa zaidi ya siku mbili na waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, ambaye amekubali kuhudhuria mkutano huo.
Kujihusisha kwa Iran kunamaanisha nchi zote ambazo zimetajwa kuhusika kwenye vita hivyo vya syria,zitahudhuria kongamano hilo la kimataifa litakalofanyika mjini Montreuz nchini Uswizi siku ya Jumatano.
Tangazo hilo la Iran limetoa matumaini katika juhudi za kusitisha vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu, baada ya baraza la upinzani la Syria SNC kuamua kuhudhuria.
Mazungumzo kati ya serikali ya rais Bashar al assad na upinzani yanatarajiwa kuanza mjini Geneva siku ya Ijumaa.
Fedha za Iran na Saudia Arabia
Iran ni mfadili mkubwa wa fedha na vifaa vya kijeshi kwa serikali ya rais Bashar al Assad.
Bwana Ban pia ametuma mwaliko sawa na huo kwa serikali ya Saudi Arabia, ambayo hufadhi upinzani nchini Syria.
Akiongea na waandishi wa habari katibu huyo mkuu wa umoja wa mataifa amesema, wameafikiana na waziri wa mambo ya nje wa Iran, kuwa dhamira kuu ya mazungumzxo hayo, ni kuunda kwa makubaliano, serikali ya mpito itakayokuwa na mamlaka.
Serikali ya Marekani na mataifa mengine ya Magharibi yalikuwa yamepinga Iran kuhudhuria mkutano huo ikiwa itakataa kuidhinisha azimio lililosainia na mataifa yenye ushawishi mkubwa duniani tarehe thelathini juni mwaka wa 2012.
Azimio hilo liliidhinisha kubuniwa na serikali ya mpito nchini Syria.
Lakini serikali ya Iran imesema kuwa itaakilishwa kwenye mkutanio huo mradi hamna vikwazo vyovyote.