Mjumbe wa Syria katika mazungumzo ya awamu ya pili ya Geneva, asisitiza kuwa hakuna kuunda serikali ya mpito na makundi ya kigaidi


Katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon,akiwa na wajumbe wengine wa umoja huo kwenye mkutano wa Geneva kuhusu Syria
Na Ali Bilali
Majibizano makali kati ya serikali ya Syria na muungano wa upinzani nchini Syria yameshuhudiwa katika siku ya kwanza ya mazungumzo ya amani ya Syria yaliyofunguliwa leo Jumatano mjini Geneva nchini Uswisi huku wakishiriki wajumbe kutoka mataifa zaidi ya arobaini na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.Ufunguzi wa mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Marekani, Urusi na Mataufa ya Ulaya pamoja na yale ya Mashariki ya Kati.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito kwa wajumbe kutoka kila upande kutumia nafasi hiyo kujaribu kuoata suluhu ya mzozo unaoendelea katika taifa lao na ambao umesababisha zaidi ya watu laki moja kupoteza maisha kwa kipindi cha miaka mitatu.

Naye Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema kuwa haitawezekana kwa rais Bashar Al Assad ambaye anatuhumiwa kutekeleza mauaji dhidi ya raia wake kuwa katika serikali ya mpito itakayoundwa.

Waziri wa Mambo ya nje wa Syria anayeongoza wajumbe wa serikali Walid Muallem wakati wa hotuba yake ya ufunguzi akionekana mwenye hasira aliyashtumu mataifa ya Magharibi kuchochea machafuko yanayoendelea katika taifa lake, na kuwaita waasi magaidi wanaotumiwa na mataifa hayo.

Ahmad Jarba kiongozi wa muungano wa upinzani ameitaka serikali ya Syria kutia saini mkataba wa kuundwa kwa serikali ya mpito na rais kuacha madaraka ili kuinusuru nchi hiyo.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na wa Urusi Dimitri Lavrov ambao ndio wadhamini wa majadiliano hayo, wamesema hii ni hatuwa kubwa muhimu na ambayo itachukuwa muda mrefu.

Hata hivyo viongozi hao wametofautiana kuhusu undwaji wa serikali ya mpito ambapo Marekani inasema rais Assad hawezi kupewa mamlaka ya kuwaongoza wananchi ambao amekuwa akiwateketeza kwa kuwashambulia kwa mabomu, jambo ambalo Urusi imeupilia mbali
www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company