Jumuia ya kimataifa imelaani vikali shambulio la kujitolea mhanga kwenye mkahawa wa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, ambao liliuwa watu kama 21 - wengi wao wageni.
Waziri wa mambo ya ndani wa Afghanistan, Mohammad Omar Daudzai, amesema maafisa kadha wa serikali ya mitaa wamesimamishwa kazi na uchunguzi unafanywa.
Kati ya waliokufa ni afisa mkuu wa Shirika la Fedha la Dunia, IMF, nchini Afghanistan, Wadel Abdallah, pamoja na wafanyakazi wanne wa Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani shambulio hilo kuwa kitendo cha kutisha.
Mkahawa huo uko katika mtaa wa Kabul wa watu wanaojiweza na ukipendwa na wageni na maafisa wa serikali.
Taliban wamesema wamehusika na shambulio hilo.
Wageni 13 kutoka Marekani, Canada, Urusi, Libnan na Uingereza wameuwawa - na wengine ni raia wa Afghanistan.
Taarifa zinasema kuwa mshambuliaji alijilipua kwenye mlango wa mkahawa.
Baada ya mlipuko watu wawili waliwafyatulia risasi wateja