Pigo kwa waasi Sudan Kusini


Maelfu ya wakimbizi wa ndani waimeutoroka mji wa Bor kutokana na vita kati ya waasi na serikali
Serikali ya Sudan Kusini inasema kuwa jeshi lake limekomboa mji wa Bor kutoka kwa waasi wa Riek Machar.

Msemaji wa jeshi Philip Aguer, amesema kuwa wanajeshi wa Sudan Kusini waliwashinda zaidi ya waasi, elfu kumi na tano wanaomtii Machar ambaye alikuwa makamu wa Rais wa zamani wa Rais Salva Kiir kabla ya wawili hao kutofautiana.

Bwana Aguer, ameelezea kwamba hatua ya jeshi kuukomboa mji huo, imeondoa wasiwasi wa waasi hao kuufikia mji mkuu Juba ambao uko Kusini mwa Bor.

Mji wa Bor umetekwa mara kadhaa tangu vita vya Sudan Kusini kuanza na kudumu kwa mwezi mmoja sasa.

Mwandishi wa BBC mjini Juba anasema kuwa jeshi sasa litaangazia zaidi kuukomboa mji wa Malakal ambao uko Kaskazini mwa nchi unaodhibitiwa kwa sasa na waasi katika juhudi za kuikomboa miji yote inayodhibitwa na waasi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company