ARSENAL imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanja wa White Hart Lane mjini London jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Shukrani kwake Tomas Rosicky aliyefunga bao hilo dakika ya pili tu akimalizia pasi ya Alex Oxlade-Chamberlain na sasa The Gunners inatimiza pointi 62 baada ya mechi 29, sawa kabisa na Liverpool iliyo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Hata hivyo, Arsenal inakaa nafasi ya tatu kwa kuzidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa na Liverpool, huku Chelsea ikibaki kileleni kwa pointi zake 66 za mechi 30 na Manchester City ni ya nne kwa pointi zake 60 kutokana na mechi 27.
Lukas Podolski akifumua shuti
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Adebayor kulia akibinuka tika tak