Steven Gerard alifunga mikwaju miwili ya penalty na kukosa ya tatu Liverpool ikiendelea kuimarisha matokeo yake baada ya kuwacharaza mabingwa watetezi wa ligi ya uingereza Machester United tatu bila katika uga wao wa nyumbani Old Trafford.
Katika kile kilichoonekana kama harakati za kushinda taji lao la kwanza tangia mwaka 1990,Liverpool ilipita mtihani wao kwa kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya timu ya Manchester United ambayo haikuweza kuwadhibiti wapinzani wao na hivyobasi kusogea hadi nafasi ya pili na pointi nne nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Chelsea.
Nahodha wa Liverpool Gerard alionyesha uongozi wake huku wakifazawadiwa mikwaju ya penalty katika vipindi vyote viwili huku timu hiyo ya meneja Brenda Rodgers ikitawala dhidi ya timu ya Machester ambayo inahitaji marekebisho makubwa.
Kutokana na mechi hizo za leo Chelsea iko katika nafasi nzuri ya kushinda taji hilo kwa alama 66 ikiwa imecheza mechi 30 huku timu za liverpool na Arsenal zikiwa na pointi 62 kila mmoja, lakini liverpool inashikilia nafasi ya pili kwa wingi wa mabao.
Arsenal ni ya tatu huku Manchester City iliocheza mechi 27 ikiwa na pointi 60 na hivyobasi ikifunga udhia wa time nne bora.