NA MUHIBU SAID
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,Kajubi Mukajanga.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Kajubi Mukajanga, amesema Bunge hilo linakabiliwa na hatari ya kutofikia malengo yake, kutokana na baadhi ya wajumbe kutaka kuingiza ushindani wa siasa.Mukajanga, aliliambia NIPASHE kuwa mwenendo wa Bunge hilo unaonyesha kuwa tahadhari iliyotolewa na baadhi ya viongozi wa kitaifa, ikiwa ni pamoja na kuzungumzia umuhimu wa wajumbe wa Bunge hilo kuweka U-vyama pembeni, haijasaidia kitu.
“Hilo linatutatiza sana sana sisi, ambao hatujatoka kwenye vyama, ambao ni wengi. Ushindani wa siasa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unataka kuingizwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba. Na hiki ni kitu hatari sana. Sababu Bunge Maalumu la Katiba ni maridhiano, siyo mashindano,” alisema Mukajanga.
Alishauri Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, kutoa nafasi ya kuchangia mijadala katika Bunge hilo kwa ulinganifu na kuepuka kupendelea upande mmoja pekee.
Alisema kwa mfano, wiki iliyopita kabla kifungu cha Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalumu kinachowazuia waandishi wa habari kuingia kwenye kamati 12 za wajumbe wa Bunge hilo zitakazojadili Rasimu ya Katiba, alisimama bungeni mara saba kuomba kuzungumzia jambo hilo, lakini hakupewa fursa hiyo.
Mukajanga alisema suala la wanahabari kuingia kwenye kamati hizo siyo la kisheria, kwani wakifanya hivyo hawavunji katiba wala sheria.
“Tusiporidhiana tutapeleka nini kwa wananchi? Zinahitajika busara na ustahamilivu na kuondokana na Bunge U-vyama. Hili ni la maridhiano,” alisema Mukajanga.
CHANZO: NIPASHE
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago