Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akiambatana na Mwenyekiti wa Kampeni wa Chalinze (CCM),Saleh Mpwimbwi (kushoto) pamoja na Msafara wake wakielekea kuhani Msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete na ujumbe wake wakishiriki kwenye dua ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa kisomo cha kumuombea Marehemu ambaye ni Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman (alieketi nyuma ya mgombe) mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (aliesimama kulia) akizungumza machache wakati alipofika kuhani msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.
"Kijana wangu,hapa ndipo ilipokuwa Ngome ya Baba yako na sie tunaimani na wewe" alisikika akisema Mzee huyu kumwambia Mgombea Ubunge,Ridhiwani Kikwete wakati alipofika kuhani Msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akimfariji Mzee Mashaka Athuman aliefiwa na Mwanae.
Ridhiwani Kikwete akisalimiwa kwa furaha.
"Iyenaaa iyenaaaa..... Iyena Inyenaaaaa...... CCM ni Nambari 1.....
Wazee wa Kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze,wakisikiliza kwa makini Sera za Mgombea wao.
Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo,Kombo Kamote akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.ambapo amewataka wananchi hao kuweka vyema Shahada zao za kupigia kura ili siku ya uchaguzi ikifika wampigie kura Ridhiwani Kikwete.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Rupungwi Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.
Wananchi wakimsikiliza Mgombea wao.
Ridhiwani Kikwete ni msikivu kwa kila mtu, bila kujali rika.
Wananchi wa Kijiji cha Mandela,Kata ya Mandela wakiwa wametulia kwa umakini mkubwa kabisa kumsikiliza Mgombea Ubunge wao.
Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wanaMandela.
Mgombea Ubunge Chalinze,Ridhiwani Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mandela.
Walipata wasaa wa kutembelea Jengo la zamani la waasisi wa TANU,ambalo sassa lipo katika hali mbaya.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Mh. Ahmed Kipozi akisalimiana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete.
Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wananchi na wanaCCM wa Msata.
WanaMsata wakifuatilia Mkutano kwa umakini kabisa.
Waliokuwa wanachama wa Chadema wakionyesha kadi zao kabla ya kuzibabidhi kwa Mgombea.
Sasa umeingia CCM.
Mtu wa watu.
Diwani wa Kata ya Lugoba akiwahutubia wana Lugoba.
Mbunge wa Jimbo la Longido,Mh. Lekule Laiza
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka akiwaomba Wananchi wa Lugoba,Jimbo la Chalinze kutofanya makosa kwenye Uchaguzi Mdogo ndani ya Jimbo lao na Wampigie Kura Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete. Sendeka aliyasema hayo jana Machi 17,2014 katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoni wakati alipopita kuwasalimia WanaChalinze.
Wewe ni wa Chalinzeeeee
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka akiwaomba Wananchi wa Lugoba,Jimbo la Chalinze kutofanya makosa kwenye Uchaguzi Mdogo ndani ya Jimbo lao na Wampigie Kura Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete. Sendeka aliyasema hayo jana Machi 17,2014 katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Sokoni wakati alipopita kuwasalimia WanaChalinze.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka akiongoza kikao watu wa jamii ya Wafugaji wa Mkoa wa Pwani.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa katika Mkutano na Wazee wa Kimasai walipokuwa wakijadilina juu ya swala la Wafugaji wa Chalinze na Pwani kwa Ujumla,jana Machi 17,2014 kwenye Ukumbi wa Masai,Chalinze.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa amekabidhiwa fimbo ikiwa ni ishara ya kusimikwa na kuwa Laigwanani wa Kimasai na Laigwanan Ole Masinga,jana Machi 17,2014.