Siku ya kimataifa ya wanawake yaadhimishwa kote Duniani

Kauli mbiu ya mwaka huu kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake ni ;“ Usawa kwa wanawake ni maendeleo kwa wote.”
Wanawake wa Malaysia wakivalia mavazi ya kitamaduni washerehekea siku ya kimataifa ya wanawake duniani.
Siku ya kimataifa ya wanawake inaadhimishwa kote duniani leo Jumamosi. Umoja wa Mataifa umesema siku hii ni ya kutafakari juu ya hatua za kimaendeleo ambazo wanawake wamepiga, kupongeza juhudi za wanawake wa kawaida kutokana na mchango wao katika historia ya maendeleo ya nchi zao na jamii zao.
Kijana mwanaharakati wa kike kutoka Pakistan Malala Yousafzai, akizungumza na idhaa ya Deewa ya Sauti ya Amerika, alisema ushauri wake kwa wanawake na wasichana kote duniani, ni kuzungumza kwa sauti kutetea haki zao. Alisema wasipozungumza sauti zao hazitasikika, lakini ikiwa wanataka kuona maendeleo na maisha bora ya baadaye sharti wasikike.

Kauli mbiu ya mwaka huu kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake ni;“Usawa kwa wanawake ni maendeleo kwa wote.” Kauli mbiu hii inasisitiza usawa wa kijinsia, kuwawezesha wanawake, kuwapa haki zao za kibinadamu, kutokomeza umasikini na kuwainua katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company