Tume Huru ya Uchaguzi ya Iraq imetangaza kuwa, asilimia 60 ya wananchi waliotimiza masharti ya kupiga kura walishiriki uchaguzi wa Bunge uliofanyika nchini humo hapo jana.
Miqdad al Shuraidi afisa wa ngazi za juu wa tume hiyo amewaambia waandishi habari mjini Baghdad kuwa, asilimia 60 ya zaidi ya Wairaqi milioni 20 walishiriki uchaguzi huo kwa ajili ya kuwachagua wabunge kutoka mikoa yote ya nchi hiyo wanaowania viti 328 vya Bunge.
Wananchi wa Iraq walijitokeza kushiriki uchaguzi huo wa jana, licha ya vitisho vya magaidi wenye mfungamano na kundi la al Qaida kwamba wangevuruga zoezi hilo.
Uchaguzi wa Bunge la Iraq unahesabiwa kuwa tukio muhimu zaidi la kisiasa nchini humo, ambapo mrengo wa kisiasa utakaokuwa na wawakilishi wengi zaidi bungeni ndio utakaobeba jukumu la kumteua waziri mkuu ambaye ataunda serikali mpya.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago