Ayatullahil Udhma Nassir Makarim Shirazi mmoja kati ya wanazuoni wakubwa nchini Iran amekosoa hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya watu karibu 700 nchini Misri na kusema kuwa vitendo kama hivyo vinairahisishia Israel kuwafanyia ukatili Wapalestina.

Akizungumza katika mji mtakatifu wa Qum, Ayatullahil Udhma Makarim Shirazi amelaani hukumu hiyo iliotolewa hivi majuzi na korti ya Misri ya kuwahukumu kifo wafuasi 683 wa harakati ya Ikhwanul Muslim. Mwanauzoni huyo pia amewalaumu viongozi wa kidini wa al Azhar kwa kutosema chochote juu ya suala hilo na kukosoa vyombo vya habari vya Misri kwa kufumbia macho hukumu hiyo.

Jumatatu iliyopita kiongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslim Mohammed Badie pamoja na wafuasi wengine wa kundi hilo walihukumiwa adhabu ya kifo kwa makosa eti ya kushiriki au kuhamasisha maandamano yanayopinga mapinduzi ya kijeshi yaliyoiondoa madarakani serikali iliyochaguliwa na wananchi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company