Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba akifungua kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya leo kutoka kulia ni mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (MNEC) kutoka Ludewa Elizabeth Haule.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe kimempongeza mbunge wa jimbo hilo Deo Filikunjombe kwa jitihada zake mbali mbali za utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo hilo.
Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Stanley Kolimba wakati akifungua kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya mjini Ludewa leo
Kolimba alisema kuwa mbunge utendaji kazi wa mbunge huyo umeendelea kuwa chachu ya kimaendeleo katika jimbo hilo na kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na imani kubwa na CCM.
Alisema mbunge huyo amekuwa mfano wa kuigwa katika kufanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM na kudai kuwa jitiihada kubwa zinazofanywa na Filikunjombe zitasaidia kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na mapenzi zaidi na CCM.
"Kweli mbunge wetu amekuwa ni mfano wa kweli katika kufanikisha maendeleo ya jimbo letu na wilaya na hata majirani wamekuwa wakipongeza utendaji kazi wake "
Katika hatua nyingine CCM wilaya ya Ludewa kimewapa pore wananchi wa kata ya Rupingu ambao wamepatwa na majanga ya mali zao mbali mbali yakiwemo mazao kuharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
"Mbali ya mvua zinazoendelea kunyesha kusaidia kutupa neema ya mazao yetu ila wenzetu wa Rupingu wamepatwa na majanga makubwa kutokana na mvua hizo hivyo tunawapa pore kwa majanga haya yaliyowakuta."
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Ludewa walipongeza jitihada za serikali ya awamu ya nne na jitihada za mbunge wao katika suala zima la uboreshaji wa miundo mbinu katika wilaya hiyo ya Ludewa kutokana na kuwa na miundo mbinu rafiki isiyosumbua sana ukilinganisha na maeneo mengine.
Pia waliiomba serikali kwa mwaka huu kuangalia uwezekano wa kutenga bajeti kubwa zaidi ya fedha kwa ajili ya ununuzi wa mahindi ya wananchi wote kutokana na kuwepo kwa dalili nzuri zaidi ya wakulima katika wilaya hiyo kupata mazao zaidi ukilinganisha na miaka iliyopita.
Kwani walisema kutokana na jinsi ambavyo wakulima wengi walivyopata mazao na kulima zaidi upo uwezekano wa wakulima kukosa soko la mazao yao yote ama wenye fedha ndio watakaonufaika zaidi na soko hilo.
Kwa upande wake, Mbunge Filikunjombe aliipongeza serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa kuendelea kuboresha maisha ya wana Ludewa kwa kufungua milango mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuanza uboreshaji wa miundo mbinu ya wilaya hiyo.
Kwani alisema mbali ya kuanza uboreshaji wa miundo mbinu hiyo tayari wilaya ya Ludewa kwa mara ya kwanza toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 kwa kipindi hiki ambacho amekuwa mbunge wa jimbo hilo tayari wananchi wa Ludewa wameanza kuona ujenzi wa barabara ya lami ukianza pamoja na wananchi wa pembezoni ambao hawajafanikiwa kuwa na umeme hivi sasa zoezi la kuwafikishia umeme limeanza. (CHANZO:BLOG YA FRANCIS GODWIN)
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago